Habari

Marekani yaiwekea vikwazo Jeshi la China, sababu hizi zatajwa

Marekani yaiwekea vikwazo Jeshi la China, sababu hizi zatajwa

Marekani imeliwekea vikwazo jeshi la China kufuatia hatua zake za kununua ndege za jeshi kutoka Urusi pamoja na makombora ya kurushwa kutoka ardhini. Inasema ununuzi kama huo unakiuka vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi kujibu, tabia za Urusi nchini Ukraine na madai ya kuingilia kati uchaguzi wa Marekani.

Majuzi China ilinunua ndege 10 za Sukhoi Su-35 na makombora ya S-400. China haijajiunga kwenye vikwazo ilivyowekewa Urusi kutoka Marekani na washirika wake tangu mwaka 2014. Uhusiano kati ya Marekani na Urusi ulidorora kwa haraka baada ya Urusi kulimega eneo la Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014.

Kwa mjibu wa BBC, Madai ya Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 na kuhusika kwake kijeshi nchini Sryria kuliongeza zaidi misukosuko. Idara ya kuunda bidhaa ya China (EDD) na mkuu wake Li Shangafu wamewekewa vikwazo kwa kufanya biashara na kampuni ya China, Rosoboronexport.

EDD na Bw Li wamejumuishwa kwenye orodha ya watu wanaowekewa vikwazo ikimaanisha kuwa mali yote wako nayo nchini Marekani yanatwaliwa na kwamba raia wa Marekani wanazuiwa kufanya biashara nao. Zaidi na hilo EDD inanyimwa leseni ya kuuza bidhaa nje na kutolewa kwenye mfumo ya fedha wa Marekani.

Marekani pia iliwaorodhesha watu wengine 33 na mashirika yanye uhusiano na jeshi la Urusi na ujasusi.Mwanasiasa mmoja nchini Urusi alisema vikwazo vya Marekani havitakuwa na madhara kwa mauzo ya ndege zake na makombora.

“Umiliki wa vifaa vya kijeshi ni muhumu sana kwa China,” alisema. Asia ni soko muhimu sana kwa watengenezaji wa silaha wa Urusi na inaripotiwa kuchukua asilimia 70 ya soko la bidhaa zao tangu mwaka 2000. India, China na Vietnam ndio wanunuzi wakuu wa silaha za Urusi eneo hilo kwa mujibu wa ripoti mpya.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents