Tupo Nawe

Marekani yaizidi China kwa idadi ya maambukizi a virusi vya Corona

Marekani imeripoti jumla ya maambukizi 85,594 na kuwa nchi yenye maambukizi mengi zaidi ikiizidi China yenye maambukizi 81,340 na Italia yenye maambukizi 80,589

Hata hivyo italia bado inaongoza kwa vifo vilivyotokana na #Covid_19, ikiwa imetangaza vifo 8,215 ikifuatiwa na Uhispania yenye vifo 4,365 huku Marekani ikiwa na vifo 1,300 na China kuna vifo 3,292

Huko Chicago katika Gereza la Cook County lenye Wafungwa 5,400, Wafungwa 24 wamepatikana na mambukizi ya virusi vya #corona baada ya Wafungwa 89 kuonesha dalili kama za mafua na kupimwa

Aidha, Meya wa Los Angeles Eric Garcetti ameonya kuwa kwa namna maambukizi yanavyoongezeka California yenye maambukizi 4,044 inaelekea kuwa New York huku New York yenye maambukizi 38,977 inaenda kuwa kama Italia.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW