Habari

Marekani yakerwa na Urusi baada ya ndege zake za kivita kutua Venezuela taifa linalopatikana Amerika Kusini

Maafisa wakuu wa Urusi na Marekani wamejibizana baada ya ndege mbili kubwa za kuangusha mabomu za Urusi kutua nchini Venezuela, taifa linalopatikana Amerika Kusini.

Tupolev Tu-160 ikiwa uwanja wa ndege wa Maiquetia, Simón Bolívar kaskazini mwa Caracas, Desemba 10, 2018

Ndege hizo mbili zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia

Ndege hizo za kivita aina ya Tu-160 zilitua Venezuela Jumattau katika kile kinachoonekana kama jaribio la kuonyesha uungaji mkono wa Urusi kwa rais wa Kisoshialisti wa Venezuela Nicolás Maduro ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema kitendo hicho ni sawa na “serikali mbili fisadi kufuja mali ya umma.”

Serikali ya Urusi imesema maneno yake hayo “hayafai hata kidogo.”

Ndege hizo mbili za kivita zenye uwezo wa kusafiri mwendo mrefu bila kutua zilitua katika uwanja wa ndege wa Simón Bolívar viungani mwa mji mkuu wa Venezuela, Caracas, zikiandamana na ndege nyingine mbili za Urusi.

Venezuela na Urusi zimekuwa marafiki kwa muda mrefu na ndege hizo mbili za kivita ziliwahi kutumwa tena taifa hilo mwaka 2008, zikiwa pamoja na manowari moja yenye uwezo wa kurusha makombora.

Ndege hizo zilifika tena Venezuela mwaka 2013.

Kitendo cha sasa kimetokea siku chache tu baada ya rais Maduro kukutana na Rais Vladimir Putin mjini Moscow.

Waziri wa Ulinzi wa Venezuela Vladimir Padrino alisema ndege hizo ni sehemu ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Venezuela na mshirika wake Urusi.

“Hili tunalifanya kwa pamoja na marafiki zetu, kwa sababu tuna marafiki duniani ambao hutetea na kuheshimu uhusiano wa usawa.”

Map showing emigration routes

“Tunajiandaa kuilinda Venezuela hadi hatua ya mwisho ikilazimu,” alisema waziri huyo akionekana kurejelea tuhuma za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali ya nchi hiyo kwamba yapo mataifa yanayotaka kupindua serikali ya nchi hiyo.

Rais Maduro alisema Jumapili kwamba kuna juhudi zinazoendelea kwa sasa “zikiratibiwa moja kwa moja kutoka White House (Marekani) za kuvuruga maisha ya kidemokrasia Venezuela na kutekeleza mapinduzi dhidi ya serikali iliyochaguliwa kikatiba, kidemokrasia na iliyo huru ya taifa letu.”

Bw Pompeo alishutumu kitendo cha kutumwa kwa ndege hizo za Urusi kwenye Twitter.

Pompeo

Msemaji wa Rais wa Urusi Vladimir Putin, Dmitry Peskov, amesema tamko la Pompeo si la kidiplomasia hata kidogo.

Bw Pompeo hakuwa afisa pekee wa Marekani aliyeshutumu kitendo hicho cha Urusi.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Kanali Rob Manning alisema hivi majuzi, Marekani ilituma meli ya jeshi la wanamaji inayotumiwa kama hospitali Amerika Kusini kutoa msaada wa kimatibabu kwa mamilioni ya raia wa Venezuela ambao wameikimbia nchi yao kutokana na mfumko mkubwa wa bei ya bidhaa na huduma na uhaba mkubwa wa bidhaa, chakula na dawa nchini mwao tangu mwaka 2014.

A Venezuelan woman who has emigrated carries a bag along the Pan-American highway

“Hii ni tofauti sana na Urusi, ambao hatua yao kutatua mgogoro huu wa kibinadamu Venezuela ni kutuma ndege za kuangusha mabomu badala ya msaada wa kibinadamu,” amesema Kanali Manning kwa mujibu wa kituo cha habari cha NBC.

Lakini Urusi siyo pekee iliyotuma ndege za kivita katika taifa au mataifa mengine.

A Russian Air Force pilot is pictured at Maiquetia International Airport, just north of Caracas, on December 10, 2018.

Marekani pia ilituma ndege za kivita nchini Ukraine, moja ya washirika wake, baada ya uhusiano wake na Urusi kudorora hasa baada ya Urusi kumega eneo la Crimea mwaka 2014.

Urusi ilichukulia hatua ya Marekani na mataifa ya Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi (Nato) ya kujenga ushirikiano wa karibu na Ukraine kwama tisho kwake.

A Russian Tu-160 bomber near Caracas, Venezuela. Photo: 10 December 2018

  • Hufahamika kama White Swans nchini Urusi (lakini zimepewa jina la utani la Blackjacks na Nato)
  • Ni ndege zenye mabawa yanayoweza kuyumba-yumba na zinaweza kwenda kwa kasi mara mbili zaidi ya kasi ya sauti
  • Ndege za kwanza zilizinduliwa mwaka 1981, lakini zikaboreshwa miaka ya 2000
  • Zinaweza kusafiri umbali wa 12,000km (maili 7,456) bila kutua
  • Zinaweza kubeba makombora na mabomu ya nyuklia
  • Zilitumiwa na Urusi katika vita Syria kuanzia mwaka 2015

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents