Habari

Marekani yakiri ndege yake kutunguliwa na majeshi ya Iran 

Jeshi la Marekani limekiri Ndege yake kutunguliwa na jeshi la Iran ilipokuwa kwenye anga ya kimataifa eneo la mpaka kati ya ghuba ya Oman na Uajemi, maafisa wa Marekani wameeleza.

Ndege isiyo na rubani iliyodunguliwa

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Awali vikosi vya kijeshi vya Iran vilidai kuwa vimeshambulia ndege ya kijasusi isiyo na rubani kwenye anga la Iran. Vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti tukio hilo dhidi ya ndege isiyo na rubani walioiita RQ-4 Global Hawk, kusini mwa jimbo la Hormozgan.Ndege isiyo na rubani iliyodunguliwa

Jeshi la Marekani awali halikuthibitisha kama ndege yake imeangushwa, huku msemaji akikana taarifa kuwa ndege ya Marekani ilikua kwenye anga la Iran.

Tukio hilo limetokea siku kadhaa baada ya wizara ya ulinzi ya Marekani kusema kuwa watapeleka vikosi 1,000 zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati baada ya kutokea mvutano kati ya Marekani na Iran.Ndege isiyo na rubani inayodaiwa na Iran kuwa ya Marekani

Shirika la Habari la Iran lilichapisha picha hii sambamba na ripoti yake

Marekani iliishutumu Iran kushambulia kwa mabomu meli za mafuta katika Ghuba ya Oman.

Mzozo huo ulishika kasi siku ya Jumatatu wakati Iran iliposema kuwa itazidisha kiwango cha urutubishaji wa madini ya Urani kinyume cha makubaliano na mataifa yenye nguvu duniani mwaka 2015.

Iran imefikia uamuzi huo baada ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani.

Msemaji wa jeshi nchini Marekani awali aliiambia Reuters kuwa ”hakuna ndege iliyokuwa ikiruka kwenye anga la Iran leo” lakini hakutaka kuzungumza zaidi.

Ramani ya Iran

Kwa nini kuna mvutano?

Mgogoro ambao umekuwepo baina ya nchi hizo mbili tangu mwaka jana wakati rais Trump alipojitoa katika mkataba wa kimataifa wa mwaka 2015 uliolenga kumaliza mpango wa nyuklia nchini Iran.

Jambo la kuona makubaliano hayo kuwa na kasoro, Trump aliamua kuweka vikwazo.

Iran iliamua kuacha kutekeleza kile ambacho iliahidi kufanya mwanzoni mwa mwezi wa Mei na kutishia kuanza kutengeneza tena nyukilia.

Meli na ndege za jeshi zilizotumwa nchini Iran ambazo wafanyakazi wake sio wa dharura wametakiwa kuondoka.Mkuu wa IAEA Yukiya Amano ameelezea wasiwasi wake kuhusu mvutano uliopo kuhusu mpango wa nyukilia wa Iran

IAEA imesema nini?

Sikiu ya Jumatatu, mkuu huyo wa Shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki, IAEA,Yukiya Amano alithibitisha kuwa Iran imeongeza uzalishaji wa madini ya kutengeneza silaha.

Lakini alikataa kutoa maelezo zaidi kuhusu suala hilo japo aliongeza kuwa hawajabainisha ikiwa madini iliyozalishwa kufikia sasa imepita kiwango kilichowekwa.

Aliiambia Bodi ya usimamizi ya IAEA kuwa ni vyema Iran ihakikishe inatekeleza mkataba wa kimataifa wa nyukilia kikamilifu.

Tahadhari ya Ndege na Meli

Wakati viongozi kutoka pande zote mbili wamesisitiza kuwa hawataki vita itokee, lakini bado mvutano ni mkubwa.

Wanadiplomasia kutoka Marekani wametoa tahadhari kuhusu ndege za kibiashara ambazo zinaenda katika maeneo hayo kuwa ziko hatarini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents