Habari

Marekani yarusha ndege za kivita Korea Kaskazini kuonesha ubabe

Ndege za kijeshi za Marekani zimepaa karibu na pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini katika kuonyesha ubabe wa kivita, baada ya nchi hiyo kuendelea kutengeneza silaha za kinyuklia na kukaidi agizo la Umoja wa mataifa.

Tarifa hizo zimethibitishwa na idara ya Ulinzi nchini Marekani kupitia kwa msemaji wake mkuu Dana White. ”Hatua hiyo ni kuonyesha kuwa rais Trump ana njia tofauti za kijeshi kushinda vitisho vyovyote”.imeeleza taarifa.

”Hili ni eneo ambalo jeshi lolote halifai kupitia na ni ndege za kijeshi za Marekani ambazo zimeweza kulifikia katika karne ya 21, licha ya tabia mbaya ya Korea Kaskazini”, amesema Bi White kwenye Taarifa kwa Vyombo vya Habari.

Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa zikirushiana maneneo katika kipindi cha hivi karibuni kutokana na vitendo vya majaribio ya silaha za nyuklia vinavyotekelezwa na Korea Kaskazini.

SOMA ZAIDI- Jaribio la siri la nyuklia nchini Korea Kaskazini laleta tetemeko la ardhi

Katika mkutano wa umoja wa mataifa siku ya Jumanne, Rais wa Marekani, Donald Trump alisema kuwa ataiangamiza Korea Kaskazini iwapo Marekani italazimika kujitetea na washirika wake.

Mpaka sasa Korea Kaskazini haijajibu chochote juu ya kitendo hicho cha kichokozi kilichofanywa na Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents