Marekani yashutumu vurugu Uganda baada ya kukamatwa Bobi Wine

Marekani imeshutumu ghasia zilizojitokeza katika mji mkuu wa Kampala na miji mingine nchini Uganda kufuatia kukamatwa kwa mgombea wa urais Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine.

Deadly protests in Uganda after Bobi Wine arrested again - The Global Herald

Ujumbe wa Marekani umesema kuwa “pande zote zipinge vita” na kuchukua hatua za kupunguza wasiwasi uliotanda nchini humo.

Bobi Wine alikamatwa wakati wa mkutano wa kampeni kwa madai ya kukiuka miongozo ya kukabiliana na virusi vya corona iliyowekwa na Tume ya uchanguzi.

Deadly protests in Uganda after Bobi Wine arrested again | Uganda | Al Jazeera

Hata hivyo, muda mfupi baadaye wafuasi wake walianza maandamano wakidai aachiliwe huru. Polisi wamesema watu watatu waliuawa huku wengine 34 wakijeruhiwa.

Uganda itafanya uchaguzi wa urais mnamo mwezi Januari 2021.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW