Habari

Marekani yasitisha kulisaidia shirika la umoja wa mataifa linaloshughulika na uzazi wa mpango, UNFPA

Marekani imejitoa kulisaidia shirika la umoja wa mataifa linalojihusisha na masuala ya uzazi wa mpango, UNFPA, na ambalo husaidia zaidi ya nchi 150.

Serikali ya Marekani imesema kuwa UNFPA hujihusisha na mpango wa utoaji mimba ambao inaupinga.

Hii ni mara ya kwanza kwa usitisishwaji wa msaada wa Marekani kwa umoja wa mataifa uliopangwa na uongozi wa Trump kutekelezwa. UNFPA imedai kusikitishwa na uamuzi huo na kwamba haijawahi kuvunja sheria yoyote.

Kwa ujumla, kiasi cha dola milioni 32.5 kimeondolewa katika mwaka wa fedha 2017. UNFPA Tanzania ni moja ya matawi yatakayoathirika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents