Habari

Mariah Carey alipwa zaidi ya bilioni 2 kutumbuiza nyimbo 3 kwenye sherehe binafsi ya mtoto wa Sultan wa Brunei

Mariah Carey ameuanza vizuri mwaka mpya 2014 kwa kuingiza pesa za chapchap, inadaiwa kuwa amelipwa $1,500,000 (bilioni 2 na milioni 300) kwaajili ya kutumbuiza katika sherehe binafsi ya mtoto wa Sultan wa Brunei Prince Azim, iliyofanyika hoteli ya nyota tano Dorchester huko London, Uingereza siku ya mwaka mpya.

Mariah Carey na Prince Azim
Mariah Carey akimuimbia Prince Azim

Inadaiwa kuwa katika sherehe hiyo Miss Carey aliimba hit zake tatu tu ikiwemo ‘Always my baby’.

Carey alipata mwaliko huo kutoka kwa bilionea Prince Azam (31) ambaye wamekuwa marafiki kwa miaka mingi.

Taarifa zinasema Mariah Carey na mume wake pamoja na watoto wao waili walitumiwa private Jet iliyowafuata Marekani kwaajili ya kuhudhuria sherehe hiyo.

Hata hivyo pamoja na mwakilishi wa Mariah kuthibitisha kuwa aliperform katika sherehe hiyo lakini alikataa kusema kiasi alicholipwa,
“It was a private party so we don’t discuss the fee. Mariah has known Prince Azim for many years. They are friends and have done a lot of charity work together.”

Wakati akiendelea kujibu maswali alitoa majibu yaliyopelekea kujulikana kile alicholipwa,
“I don’t have any more details.’ Still, even at £1million, the appearance was relatively cheap by some stars’ standards.”

Mariah Angola
Mariah alipokuwa Angola mwaka jana akiwa na Rais Josè Eduardo Dos Santos

Hivi karibuni Mariah Carey alikuwa nchini Angola, ambako nako alilipwa dola milioni 1 (sawa na shilingi bilioni moja na nusu) kutumbuiza mbele ya Rais wa nchi hiyo Josè Eduardo Dos Santos, sherehe iliyodhaminiwa na mtandao wa simu wa Unitel unaomilikiwa na mtoto wa Rais huyo aitwaye Isabel.

Source: Mail Online

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents