Burudani

Mariah Carey amwagana na mkata viuno wake

Mariah Carey amemwagana na mpenzi wake Bryan Tanaka ambaye pia ni dansa wake.

Mtandao wa TMZ umedai kuwa mahusiano ya wawili hao yamevunjika kutokana na vitu viwili ambavyo ni wivu pamoja na Mariah kutumia fedha vibaya.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao huo kuwa Brayan hakuwa akifurahia mahusiano yaliyopo kati ya Carey na aliyekuwa mumewe Nickk Canon ambaye pia amezaa naye watoto wawili Monroe na Moroccan.

Mahusiano ya wawili hao yamedumu takribani miezi mitano pekee tangu Mariah alipoachana na bilionea James Parker mwishoni mwa mwezi October mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents