Habari

Mariah Carey awa jaji mpya wa American Idol


Hatimaye Mariah Carey ametangazwa rasmi kuwa jaji mpya wa American Idol na hivyo kuziba pengo lililoachwa na Jennifer Lopez.
Mtandao wa Us Weekly uliripoti July 12 kuwa Mariah Carey alikuwa kwenye mazungumzo na waandaaji wa show hiyo ili awe jaji kwenye msimu wa 13 wa American Idol.
Kutokana na hatua hiyo, Mariah Carey amekuwa jaji wa shindano la muziki anayelipwa fedha nyingi zaidi.
Mkataba huo aliosaini na American Idol utamuingizia dola milioni 18 kwa mwaka.
Jennifer Lopez alikuwa akilipwa dola milioni 12 wakati jaji wa shindano jingine la The X Factor Britney Spears hulipwa dola milioni 15 kwa mwaka.
“Kama muimbaji, mwandishi wa nyimbo na producer, itakuwa raha na baraka kusaidia kupatikana kipaji kipya na kurudisha kwa njia ya American Idol, mshindi huyo wa mara tano wa tuzo za Grammy alisema jana July 23 kwenye maelezo yake.
“Kwa sasa nipo studio nikirekodi albam yangu mpya na wimbo wa kwanza ‘Triumphant, utatoka mapema mwezi ujao” Carey aliongeza.
“I can’t wait to channel my creative energy as a part of this show which is a massive global phenomenon.”
Mwanzilishi wa American Idol na mtayarishaji mkuu Simon Fuller, 52, amesema “proud to have one of the world’s greatest-ever female singers join our show. Mariah defines the word ‘Idol’ and will inspire every singer that has the honor of performing in front of her.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents