Tupo Nawe

Mariah Carey na Nicki Minaj wathibitisha kutoendelea kuwa majaji wa American Idol msimu ujao

Baada ya kuwepo speculation juu ya uwezekano wa baadhi ya majaji wa shindano la American Idol kutoendelea na msimu ujao, hatimaye rapper Nicki Minaj na mwimbaji Mariah Carey wametoa misimamo yao.

Nicki & Mariah

Mariah Carey ambaye amekuwa jaji katika msimu wa 12 uliomalizika hivi karibuni amethibitisha kuwa hatakuwepo katika msimu ujao kama jaji, na kuongeza kuwa anatarajia kuanza world tour yake. Kupitia akaunti ya tweeter ya PMK.BNC walitweet, “W/ global success of “#Beautiful” (#1 in 30+ countries so far) @MariahCarey confirms world tour & says goodbye 2 Idol.” Tweet ambayo Mariah ali retweet taarifa hiyo dakika chache baadae.

Jaji mwingine ambaye amethibitisha kutoendelea na msimu ujao wa 13 wa reality show hiyo ya kusaka vipaji ni Nicki Minaj, ambaye alhamisi (May 30) alitweet “Thank you American Idol for a life changing experience! wouldn’t trade it for the world! Time to focus on the Music!!! Mmmuuuaahhh!!!”

Nicki Minaj na Mariah Carey wamefuatia kujitoa katika meza ya majaji wa shindano hilo baada ya jaji Randy Jackson aliyejiondoa wa kwanza mapema sana. Baada ya uthibitisho huu wa Minaj na Carey sasa meza hiyo imebakiwa na jaji mmoja tu Keith Urban ambaye bado hajasema chochote kama ana nia ya kubaki ama laa, japo matarajio ya wengi ni kuwa huenda akaiaga ajira hiyo pia.

Habari zilizo chini ya kapeti ni kuwa waandaaji wa American Idol wako katika mazungumzo na mwimbaji wa R&B Jennifer Hudson ili aweze kujiunga na team mpya ya majaji itakayoendesha show hiyo kwa msimu mpya wa 13.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW