Burudani

Mariam wa BSS atia huruma

Mariam_Bss_2010_face

ALIYEKUWA mshindi wa kwanza katika shindano la  Bongo Star Search 2010 maarufu kama BSS, Mariam Mohamedi hivi sasa hali yake  ya kiuchumi inazidi kuwa mbaya kisi cha kurudia rafiki zake ambao mwanzo aliwakana kwa madai kwamba thamani yake ipo juu.

 

Akiongea mmoja wa rafiki zake alidai kwamba Mshindi huyo ambaye alitwa 30 Milioni kwa sasa hali yake imekuwa ngumu kiasi cha kuuza kila kitu chake cha  thamani kwa bei chee na kubaki kama alivyokuwa mwanzo.

Alisema wakati aliposhinda hilo shindano alikuwa hataki kuongea na rafiki zake ambao mwanzo, ndiyo waliomuunga mkono kwa hali na mali mpaka kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, lakini hali ilipoanza kuwa tete, walimuona akija kwa kasi na kutaka kurudisha thamani ya urafiki waliyoipoteza.Mariam_bss

(Mariam akiimba katika tamasha la BSS)

Mdau huyo alizidi kusema hivi sasa Mariam, amekuwa akizunguka ovyo ovyo, na kuudhulia kwenye matamasha ya uswahili kwa lengo lakujipatia ridhiki. aidha alidai kwamba hali hiyo ya kimaisha imemfanya ajiunge na kikundi cha sanaa ya maigizo kilichopo huko Uswahilini, ilimradi awe Busy. Mdau alisema kwa sasa hali ya Mariam inatia huruma kwani huwezi amini kama ndiyo yeye alishika 30 milioni Desemba 2010 na na leo kuishi maisha haya kama Digidigi.

Tamasha hilo hivi karibuni linatarajiwa kuanza tena kwa msimu wa mwaka 2011, huku likichukua washiriki ambao walifanya vizuri kwenye matamasha ya BSS yaliyopita, na kuwapa nafasi nyingine ya kujaribu kutwa taji hilo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents