Michezo

Mario Mandžukić afuata nyayo za Wahispanyola Gerrad Pique pamoja na David Silva

Mario Mandžukić afuata nyayo za Wahispanyola Gerrad Pique pamoja na David Silva

Hii imekuwa ni wiki ya wachezaji kutundika daluga baada ya Gerrad Pique kutoka nchini Uhispania kuamua kutundika daluga ikafuata zamu ya Mhispania mwingine David Silva kutangaza kustaafu kuitumikia timu yake ya taifa ya Uhispania leo imekuwa zamu ya Mcroatia huyu si mwingine bali ni Mario Mandžukić .

MOSCOW, RUSSIA – JULY 11: Mario Mandzukic of Croatia celebrates victory following the 2018 FIFA World Cup Russia Semi Final match between England and Croatia at Luzhniki Stadium on July 11, 2018 in Moscow, Russia. (Photo by Alexander Hassenstein/Getty Images)

Mandžukić ameandika waraka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa anaamua kustaafu kuitumikia timu yake ya taifa ya Croatia,Mario ameongea mengi sana kuhusiana na mafanikio aliyoyapa katika taifa lake kupitia soka lakini pia kuweza kukutana na wachezaji mbalimbali.

Na haya ndio maneno yake:-

Mario Mandžukić alizaliwa miaka 32 iliyopita,May 21 ya mwaka 1982 katika nchi ya Croatia na amefanikiwa kuvitumikia zaidi ya vilabu 7 katika karia yake ya mpira vikiwemo Bayern Munich,Atletico Madrid na kwa sasa akiitumikia Juventus.

Lakini pia katika timu yake ya taifa ya wakubwa alifanikiwa kujiunga nayo  mwaka 2007 akicheza michezo 89 na akiifungia magoli 33 akiwa mfungaji wa pili wa muda wote katika taifa hilo mwenye magoli mengi akizidiwa na mkongwe Dvor Suker mwenye magoli 45.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents