Michezo

Marouane Fellaini aongeza kandarasi ndani ya Manchester United

Kiungo wa klabu ya Manchester United, Marouane Fellaini ameongeza kandatrasi yake ndani ya timu hiyo itakayo mfanya kuendelea kusalia hapo mpaka mwezi Juni mwaka 2020.

Fellaini ambaye kwa sasa yupo na timu yake ya taifa ya Ubelgiji kwenye michuano ya kombe la dunia huko nchini Urusi ametoa habari hiyo kuwa ataendelea na mashetani hao wekundu wa Uingereza.

“Ningependa kuwataarifu kuwa nitaendelea kuwa mchezaji wa Manchester United player, nimefanya maamuzi haya kwakuwa najisikia furaha kuwa hapa,” amesema Fellaini.

Mchezaji huyo pia ameongeza kuwa “Ninajiskia kuwa miongoni mwa hii timu hasa chini ya uongozi wa Jose bado tunamengi tunayo hitaji kuyafikia. Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwako Jose kwa mapenzi yako sikuzote unayoonyesha kwangu.”

Meneja wa United, Jose Mourinho amesema kuwa anajiskia mwenye furaha baada ya kuona Marouane anaendelea kusalia kwakuwa anaamini siku zote vile anavyotamani kuendelea kuwepo ndani ya klabu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents