Burudani

Martin Kadinda aeleza kwanini filamu ya Van Vicker na Wema inachelewa kutoka

Meneja wa mwanadada wa filamu Wema Sepetu, Martin Kadinda ameelezea sababu ya kuchelewa kutoka kwa filamu ya ‘Day After Death’ iliyochezwa na Wema pamoja na muigizaji wa Ghana, Van Vicker ‘Day After Death’.

1

Martin amesema filamu hiyo ilikuwa itoke September mwaka huu lakini imeshindikana kutokana na kampeni za uchaguzi.

“Filamu mpaka sasa ipo tayari, lakini movie hii hatuwezi kuiachia kama anavyoachia movie nyingine.Lazima afanye launch na ilikuwa launch ifanyike toka mwezi wa tisa lakini toka mwezi wa sita mpaka sasa Wema yupo kwenye kampeni,” Kadinda ameiambia Bongo5.

“Kwahiyo tunasubiri mpaka hizo kampeni ziishe na uchaguzi upite Wema atakuwa anazindua products zake mpya halafu baada ya hizo products kuzinduliwa ndio filamu itazinduliwa rasmi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents