Burudani

Martin Kadinda kufunga ndoa na Mmasai

By  | 

Martin Kadinda amefunguka kwa kuweka wazi mipango yake ya kufunga ndoa.

Mbunifu huyo wa mavazi hapa nchini, amesema baada ya miaka miwili kupita atatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake mwenye asili ya Kimasai.

Akijibu swali la mmoja wa wanafunzi wa vyuo mbalimbali katika chuo kikuu cha Udsm Jumamosi hii watika wa kongamano la “Her Intiative,” Kadinda amesema, “Nimekuwa nikiyaficha sana mahusiano yangu, lakini napenda kuwaambia tayari nina mtoto mmoja wa kiume. Baada ya miaka miwili kupita nitafunga ndoa na mpenzi wangu ambaye ni Mmasai.”

Meneja huyo wa zamani wa Wema Sepetu ameongeza kuwa, hapendi kuhusisha maisha yake na familia yake hata wajomba na wengine kwa watu kuweza kufahamu chochote, kwani huwa anapenda kuwa mbinafsi kwenye hilo.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments