Habari

Marufuku tamasha la watu weusi Paris

Tamasha la Nyansapo lililotarajiwa kufanyika mwezi Julai limepigwa marufuku ma Meya wa jiji la Paris kwa sababu halihusishi wanawake wakizungu.

Kwa mujibu wa meya huyo amesema kuwa asilimia 80 ya watu katika tamasha hilo inategemewa kuwa ni wanawake weusi jambo ambalo linawakataza wanawake wakizungu kuhudhuria tamasha hilo. Baadhi ya mashirika ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Ufaransa yameshutumu tamasha hilo.

Ijumaa iliyopita kiongozi wa kanda wa chama cha mrengo wa kulia National Front alimtaka Bi Anne Hiladlgo aeleze ni kwa nini hafla hiyo ya “ubaguzi wazi wa rangi” inafanyika.

Baada ya kauli hiyo, kiongozi huyo alitweet “Tutawafungulia mashtaka kwa kosa la kufanya ubaguzi”.


Meya Anne Hiladlgo

Tamasha hilo lilitarajiwa kufanyika katika eneo ambalo linamilikiwa na baraza la mji wa Paris, lakini tamasha yenyewe haliko wazi kama litafanyika tena.

Waandalizi wamesema meya huyo hana mamlaka yoyote ya kuingilia hafla hiyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents