Afya

Marufuku Wagonjwa kutazama filamu, michezo au tamthiliya Hospitalini

Serikali kupitia Wizara ya Afya, imepiga marufuku runinga zote za hospitali za serikali kuonesha wagonjwa vipindi vya kawaida kama tamthiliya badala yake waonyeshe vyenye kutoa elimu ya afya.

Image result for dkt faustine ndugulile
Dkt. Ndugulile
Marufuku hiyo, imetolewa jana Januari 14, 2019 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, alipokuwa akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Dodoma, baada ya kufanya ziara hospitalini hapo.
Tulishatoa ‘flash’ bure za vipindi vya kutoa elimu ya afya kwenye hospitali zote za serikali, sitaki kuona runinga hizo zinaendelea kuonyesha vipindi vya michezo na vinginevyo vya kawaida,” amesema Dkt. Ndugulile.
Dkt. Ndugulile kwa upande mwingine ameagiza hospitali zote za rufani nchini kuhakikisha wanafunga mifumo ya ukusanyaji taarifa za kitabibu kila idara kwenye hospitali zao.

Tunahitaji kupata taarifa za kila mgonjwa, muda aliofika, aina za vipimo pamoja na daktari aliyemhudumia na ahakikishe anasaini na taarifa zote hizo zinatakiwa kupatikana na kwenye mfumo wa aina moja,” amesema Dkt. Ndugulile.

Chanzo: Nipashe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents