Siasa

Marufuku wimbo wa Taifa kwenye simu

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika amepiga marufuku wananchi kuweka wimbo wa taifa katika simu zao za mkononi…

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika amepiga marufuku wananchi kuweka wimbo wa taifa katika simu zao za mkononi. Mkuchika alisema kufanya hivyo ni kuudhalilisha wimbo wa taifa pamoja na nchi kwa ujumla kwani inapaswa kuheshimiwa mahali popote. ‘

‘Unakuta mtu ameweka wimbo wa taifa kwenye simu yake ya mkononi halafu anapopigiwa ama yuko kwenye ulevi au mahali kwingine ambako wimbo huo hauhitajiki, hakika tunaokosesha heshima kama wimbo unaowakilisha utaifa wetu,” alisema.

Aliongeza kuwa nyimbo nyingine zinazosifu Tanzania zinaruhusiwa kutumika kwenye simu, lakini sio wimbo wa taifa. Alisema pia kuwa wizara yake inaandaa utaratibu wa kupitia sheria zetu iliiweze kuruhusu wananchi wote kutumia bendera ya taifa kama zilivyo nchi nyingine.

Waziri huyo aliyasema hayo wakati akikabidhi bendera ya taifa kwa timu ya Olimpiki inayoondoka leo mchana kwenda Beijing, China. Mkuchika aliwapa wanamichezo hao salamu kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye ameitakia timu hiyo kila la heri na kuitaka ihakikishe inarudi na medali na pia kuwa na nidhamu kwa muda wote watakapo kuwa huko.

Timu hiyo inaondoka na wanamichezo 10 wakiwemo wanariadha nane na waogeleaji wawili, akiwamo Mkuchika.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents