Michezo

Mashabiki wa Chelsea waliwashabikia Manchester United kwao huku wakimzomea kocha wao “Utafukuzwa kazi alfajiri” Sarri awajibu

Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri alisema kuwa timu yake ilicheza mchezo wa ‘Kugawanyika’ baada ya Man United kupata ushindi katika uwanja wa Stamford Bridge na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la FA.

Matokeo hayo yanauweka uongozi wa mkufunzi wa Chelsea Muitaliano Sarri katika hali mbaya , huku United ikijibu baada ya kupoteza kwa mara ya kwanza chini ya ukufunzi wa Ole Gunna Solskjear na kufanikiwa kusonga mbele huku wakipangiwa tarehe ya kukutana na Wolveshampton katika robo fainali ya kombe hilo.

Ander Herrera alifunga krosi iliopigwa na Paul Pogba na kufanikiwa kuipatia United uongozi kunako dakika ya 31 kabla ya Pogba kufunga bao la pili kupitia kichwa na kuipatia timu yake fursa nzuri baada ya krosi iliopigwa na Marcus Rushford.

Huku Chelsea wakishindwa kwa mara nyengine , mashabiki wao walimshutumu kocha wao Sarri.

Lakini pia wealiwazoma wachezaji wa ziada wakati wanatoka uwanjani na mkufunzi huyo mbali na kuifanyia mzaha filosofia yake, na kutaka kurudi kwa Frank Lampard kama mkufunzi wa timu hiyo huku wakishirikiana na mashabiki wa United kuimba ”utafutwa kazi alfajiri”.

Kwa upande wa Sarri alisema ”Tulicheza kana kwamba tumekanganyikiwa katika kipindi cha pili lakini katika kipindi cha kwanza tulionyesha mchezo mzuri”.,

”Nina wasiwasi kuhusu matokeo haya lakini sio kuhusu mashabiki kwa sababu naelewa hali yao. Ninawaelewa mashabiki wetu kwasababu matokeo hayo sio mazuri na tumetolewa katika kombe la FA”.

”Nilikuwa na wasiwasi mkubwa zaidi nilipokuwa kocha katika ligi ya daraja la pili nchini Italia lakini sio sasa”.

Solskjaer hakuwa na matatizo hayo baada ya kufurahia sifa alizokuwa akimwagiwa na mashabiki wa United baada ya kuongeza ushindi mwengine licha ya kutokuwepo kwa Jesse Lingard na Anthony Martial ambao wanauguza majeraha.

”Mchezo kwa upande wetu ulikuwa mzuru sana leo , mbinu zetu zilizaa matunda” ,alisema kaimu mkufunzi huyo wa United.”

Mashabiki wa klabu hiyo walioimba jina la mkufunzi huyo hawatakuwa na kura ya kupiga wakati uamuzi kuhusu mkufunzi mpya utakapotolewa, lakini walionyesha hisia zao katika usiku mwingine muhimu kwa mtu ambaye anatumai kumrithi Jose Mourinho kwa kandarasi ya kudumu.

Solakjaer amekabiliwa na msururu wa mitihani muhimu tangu aliporudi katika klabu ya Old Trafford baada ya kufutwa kazi kwa Mourinho katikati ya mwezi Disemba.

Mtihani wa kwanza ilikuwa jinsi angejibu matokeo duni yaliowachwa na mtangulizi wake.

Mkufunzi Sarri alianza kazi yake vizuri katika wiki za mapema za msimu huu huku Chelsea ikionekana kushindana na Manchester City na Liverpool huku kukiwa na matumaini kwamba raia huyo wa Itali alionyesha sifa nzuri katika soka ya Uingereza.

Lakini huku muda ukiyoyoma , Sarri alikabiliwa na hasira zote za Stamford Bridge huku wasiwasi ukizidi kuhusu hali ya matokeo duni ya Chelsea.

Kulikuwa na wito wa kurudi kwa Frank Lampard ambaye kwa sasa anaifunza Derby County.

Ulikuwa usiku ambao mashabiki walikosa subira huku, watu wakitoa maoni yao huku Sarri akithibitishiwa kwamba anaendelea kupoteza umaarufu miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo.

Klabu hiyo itakabiliana na Manchester City katika fainali ya kombe la Carabao siku ya Jumapili na itakuwa uamuzi muhimu kwa klabu hiyo kumfuta kazi siku chache kabla ya mechi hiyo. Bado vigumu kumuona Sarri akiponea shoka hilo.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents