Michezo

Mashabiki wa Chelsea wananitia hasira – Alvaro Morata

By  | 

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid ambaye kwa sasa anakipiga kunako klabu ya Chelsea, Alvaro Morata ameonekana kuingiwa na wasiwasi juu ya kiwango chake baada ya kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo baada ya kutokuanza vyema kwenye mechi za Pre-season na kwenye mchezo wa ngao ya jamii.

Alvaro Morata

Morata amesema maoni ya mashabiki wa Chelsea yanamfanya ajione ndiyo kwanza anaanza safari ya soka hivyo atajitahidi kuwadhihirishia uwezo wake uwanjani na kuwafanya wawe watu wa furaha daima.

“Nimecheza mechi mbili tu za pre-season, kwa dakika 15 na kukosa penati moja lakini tayari mashabiki wameanza kuniandama najua fika sababu ya kuniandama ni gharama ya usajili wangu wa kuja hapa, bila shaka maoni yananifanya nifanye kazi kwa bidii niweze kuwafurahisha, kweli maoni yao yananitia hasira ya kupambana”,amesema Morata kwenye mahojiano yake na gazeti la Marca la Hispania.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi kuu EPL, Kesho watafungua ligi kuu ya nchini England dhidi ya klabu ya Burnley katika mbio za kutetea ubingwa na Alvaro Morata anatarajiwa kuongoza mashambulizi.

By Godfrey Mgallah

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments