Michezo

Mashabiki wa Liverpool walivyoungana na mashabiki wa Bayern Munich kukemea gharama za uuzwaji wa tiketi katika mchezo wa jana

Katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya UEFA iliendelea usiku wa kuamkia leo katika michezo miwili.Mchezo mmoja ulifanyika Uingereza ambako Liverpool walikuwa wenyeji dhidi ya Bayern Munich na mchezo mwingine ulifanyika nchini Ufaransa ambako Lyon waliwakaribisha Barcelona.

Katika mchezo katika Lyon na Barcelona, wageni Barcelona walikosa nafasi chungu nzima na kushindwa kufunga hata goli moja katika mashambulio 25 iliotekeleza katika mechi ya sare tasa dhidi ya klabu ya Ufaransa Lyon.

Washambuliaji wa Barca Lionel Messi, Luis Suarez na Phillipe Coutinho ambao wamekuwa moto wa kuotea mbali dhidi ya upinzani wowote walizuiwa na kipa wa Lyon Anthony Lopes.

Lyon walikuwa na nafasi lakini Marc-Andre ter Stegen alipangua shambulio la Martin Terrier. Mechi ya marudiano itafanyika katika uwanja wa Nou Camp tarehe 13 mwezi Machi.

Wakati huohuo matumaini ya klabu ya Liverpool kufuzu katika robo fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya yalididimia baada ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munchen katika uwanja wa Anfield. Wenyeji walifanya mashambulio lakini wakashindwa kuona lango la upinzani kutokana na safu kali ya ulinzi ya Bayern.

Sadio Manne alikosa nafasi za wazi ,akipiga mpira nje licha ya kusalia na kipa. Joel Matip naye pia alishindwa kufunga krosi iliopigwa na Roberto Firmino kutoka maguu sita ya goli.

Na makosa ya Matip karibu yaipatie Bayern bao la kwanza la ugenini wakati alipokuwa akijaribu kuondosha hatari katika lango la Liverpool.

Mabingwa hao wa Ujerumani walikuwa chonjo katika safu yao ya ulinzi katika kipindi cha kwanza, huku kichwa cha Mane kunako dakika ya 85 nje ya goli ikiwa ndio shambulio la karibu sana ambalo Liverpool walifanya.

Mechi ya mkondo wa pili itachezwa katika uwanja wa Allianz Arena mnamo tarehe 13 mwezi Machi.

Mabingwa Barca wanaongoza ligi ya La Liga , wakiwa na pointi saba juu ya Atletico Madrid iliopo katika nafasi ya pili , hawajashinda kombe la Ulaya tangu 2015 wakati walipoishinda Juventus katika fainali.

Katika mechi hiyo kikosi hicho cha, Ernesto Valverde kilikuwa kikipigiwa upato kuibuka mshindi na kufuzu katika robo fainali lakini kushindwa kwao kupata bao kuliiwacha mechi hiyo kuwa wazi.

Miamba hiyo ya Catalan sasa imepata sare katika mechi zake nne kati ya tano ilizocheza katika mashindano yote na wangefunga magoli mawaili katika dakika za kwanza nne lakini Ousmane Dembele alikosa kucheka na wavu huku Lionel Messi akipiga juu baada ya kupewa mkwaju wa adhabu.

during the UEFA Champions League group B match between RSC Anderlecht and Bayern Muenchen at Constant Vanden Stock Stadium on November 22, 2017 in Brussels, Belgium.

Lakini katika hali iyoyokuwa ya kutarajiwa katika dimba la Anfield kulikuwa na sintofahamu kwa mashabiki wa timu zote hizo mbili ambako walilalamikia kuhusu gharama za kununua tiketi katika mchezo wao huo.

Mashabiki wa Liverpool na Bayern waungana jambo moja limewaunganisha mashabiki wa Bayern na Liverpool ni gharama za ticket za kuingia uwanjani. Swala limeanzishwa na mashabiki wa Bayern wakilalamika kupitia mabango kwamba gharama ya ticket ni kubwa sana.

Bango hilo lilisomeka “Away ticket: LFC £48. FCB 55€.
“Th€ gr€€d knows no £imits.
“Twenty is plenty.”
£48= Tsh 146,000. Baada ya mashabiki wa Bayern kuonyesha mabango hayo, mashabiki wa Liverpool waliwashangilia kwa makofi kuonyesha kwamba wana afiki swala hilo kwamba bei ni kubwa.

By Ally Juma


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents