Michezo

Mashabiki wa Manchester United kutumia ndege kuhimiza Moyes ‘apigwe chini’

KUNDI la mashabiki wa Manchester United linapanga kukodisha ndege itakayopeperusha kibendera chenye maandishi ya kumpinga kocha wa timu hiyo David Moyes Jumamosi. Manchester United imekuwa na msimu mbaya kiasi cha mashabiki wa timu hiyo kuanza kulalamika vikali wakimtaka Moyes afutwe kazi.

David-Moyes-Manchester-United-manager-profile_3090507

Mnamo Jumanne, shabiki mmoja alimzomea kocha huyo baada ya timu hiyo kucharazwa mabao 3-0 na Manchester City katika uwanja wa Old Trafford.

Baada ya mechi hiyo, kundi linalojiita Red Issue limejitokeza na sasa linachanga pesa za kukodisha ndege itakayopaa juu ya uwanja wa Old Trafford ikiwa imebeba kibendera chenye maandishi yanayosoma Moyes Out.

United inayoshikilia nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu, itakutana na Aston Villa katika uwanja wa Old Trafford hapo Jumamosi. Baada ya mechi hiyo, Manchester United inakabiliwa na jinamizi la kufika nusu fainali ya Uefa dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich. Vijana hao wataalika mabingwa hao wapya wa Ujerumani katika mechi ya mkondo wa kwanza wa robo fainali hapo Jumanne.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger pia anakabiliwa na presha sawa na ya Moyes na shabiki mmoja ametayarisha bango lenye maandishi Enough is Enough, Wenger Out kumaanisha ‘Tumetokuchoka, Wenger aondoke’. Mfaransa huyo hatatia saini kandarasi mkataba mpya kwani wa sasa unaisha hapo Juni.

Swahili Hub

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents