Soka saa 24!

Mashabiki wacharuka Instagram kisa picha inayomuonyesha Diamond kavaa ‘kikuku’

Mashabiki katika mtandao wa Instagram wamecharuka baada ya kuona picha inayomuonyesha muimbaji maarufu nchini Tanzania, Diamond Platnumz akiwa amevaa cheni mguuni (kikuku).

Mapema leo muimbaji huyo ambaye yupo nchini Marekani kwenye tour ya ABoy From Tandale, alipost picha zake mpya kupitia mtandao huo huku moja katika mguu wake wa kushoto akionekana kama amevaa kitu kinachohisiwa ni cheni.

Baada ya kuona picha hiyo mashabiki wengi kupitia instagram wamekasirishwa na kitendo hicho kwa madai hakiendani na tamaduni za Kitanzania.

Haya hapa chini ni maoni ya mashabiki hao, hata wewe unaweza kutoa maoni yako kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii.

Makerahabiba
Mm mmmm hadi kikuku huko sio kabisa jaribu kumtafakari na mwenyez mungu juu ya ukuu wale Leo ni raha kuvaa herein .kikuku je je ukirejea kweke mungu utamjibu kitu gani … CIO poa.

diamondpletnumz
Kwani kikuku maana yake nin? Mimi kwa mtazamo wangu nipambo kama pambo jingine tu , then kuhusu maana ya kitu hua inatengenezwa na mtu mweenyewe nikama vile kisu unaweza kukitumia kukatia nyanya na vitunguu au ukaamua kumdunga mtu

lemon_spiceup

Man_ada sio uteam..kwani huyo Si MTU mzima mtampangiaje maisha…kaamua ni yeye..who are u kumwambia what to do…tatizo wabongo chokochoko nyingi…jifunzeni kwa wazungu wenzenu kila MTU ana maisha take…who are u to judge someone wewe mangapi unafanya ambayo sio sahihi..eti?.

ishamwinyi2454.

Heee!!!😨😨😨 kikuku tenaaa!😭😭😭 innaalillah wainnaailah rajiun yaaAllah tujaaliye mwisho mwema waja wako kwan ss ni wadhalimu kwako na kwako tutarejea.


WAnaxhangaaa

Kikukuu wakat shanga unazo kiunon hawajui bila kumkatikia mzee baba pesa aziingiii😂😂😂👌👌 waambie saiv utuumii nguvu kubwa kujikaza toilet 😁😁🙌.


uwalymussa

Wachokozi Na vikuku haya sindio Mwenenu kazi kwenu Wazee wa Modo zakubana cjui vikondomu Mama yenu Ameanza watoto mutafata Sio wakwetu huyo Kiumeni hatuna Tamaduni hizi

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW