Mashabiki waiponza Denmark kwa FIFA nchini Urusi

Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani (FIFA) limeilima faini ya dola za Kimarekani 20,200 Chama cha soka nchini Denmark (DFA) kwa kushindwa kuwadhibiti mashabiki wake waliyobeba mabango ya uchochezi wakati wa mchezo wao dhidi ya Australia uliyomalizika kwa matokeo ya bao 1 – 1.

FIFA imesema kuwa mashabiki wa Denmark pia walionekana kutupa vitu upande wa Australia na kushindwa kushindwa kufuata sheria wakati kabla ya mechi hiyo kuanza ikiwa pamoja na kutoheshimu wimbo wa taifa wakati wa ufunguzi.

Denmark pia ilitozwa faini kwa mashabiki wake kubeba mabango yaliyoashiria vitendo vya ngono wakati wa mchezo huo ndani ya Samara, FIFA hutumia wachunguzi kwenye michuano hii ya kombe la dunia ili kuhakikisha jambo lolote la kibaguzi halitokei na kukomesha kabisa vitendo hivyo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW