Michezo

Mashabiki wamzawadia Mbuzi kipa wa Singida United

Mashabiki wa klabu ya Singida United wameamua kumzawadia zawadi ya Mbuzi mlindalango wa timu hiyo, Saadat Juma baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo wake wa michuano ya kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) wake dhidi ya Polisi Tanzania.

Juma ambaye ni kinda wa Serengeti boys amezawadiwa zawadi hiyo baada ya kuonyesha kiwango bora wakati timu yake ya Singida United ikiibuka na ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya Polisi Tz mchezo uliyopigwa Februari 24 katika dimba la uwanja wa Namfua.

Michuano hiyo ya kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ili endelea tena hii leo kwa mechi mbili kuchezwa kwenye viwanja tofauti.

Timu ya Stand United imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 4 – 3 dhidi ya Dodoma FC kwa njia ya mikwaju ya penati baada ya kumalizika dakika 90.

Wakati mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya Kiluvya United ambayo imekubali kipigo cha bao 1 – 0 kutoka kwa Tanzania Prisons ya Mbeya.

Baada ya kumalizika kwa michezo hiyo miwili  ya leo hizi ndiyo timu zilizo tinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya FA.
Azam FC
Young Africans
Njombe Mji FC
JKT Tanzania
Mtibwa Sugar FC na
Singida United

Stand United

Tanzania Prisons

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents