Habari

Mashambulio matatu yatokea Marekani ndani ya saa 24

Jumapili na Jumamosi kumetokea mashambulio matatu katika ardhi ya Marekani – bomu lililolipuka Manhattan, watu kuchomwa kisu huko Minnesota na bomu kulipuka kwenye bomba la maji huko New Jersey.

2016-09-18t221319z_01_aal702_rtridsp_3_new-york-blast-19-09-2016-00-09-04-791

Kuna uhusiano mkubwa na tukio la kigaidi huku watu watano wakikamatwa New York. Bomu lililolipuliwa makusudi huko New York limejeruhi watu 29.

Mamlaka zimedai kuwa hakuna ushahidi iwapo matukio hayo yalikuwa na uhusiano lakini kutokea ndani ya saa 24 kumesababisha hofu za usalama, kitu ambacho tayari kimekuwa muhimu kuzingatiwa katika mchuano wa urais kati Hillary Clinton na Donald Trump.

Bomu la pili liligundulika karibu na eneo hilo na polisi walifanikiwa kulitegua.

Kwa upande mwingine mtu aliyewachoma kisu watu tisa kwenye mall huko Minnesota Jumamosi, aliuawa na polisi ambaye hakuwa kazini. Mtu huyo amedaiwa kuwa mwanajeshi wa kundi la Islamic state.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents