Habari

Mashine ya ‘ultra sound’ yaibiwa kwenye wodi ya wajawazito Hospitali ya Bariadi

Mashine inayotumika kupima magonjwa ya ndani na kutambua taarifa katika mwili wa binadamu (utra sound), imeibwa na kwenye wodi mpya ya wajawazito Hospitali ya Wilaya ya Bariadi.

Mashine hiyo, kifaa chake cha kudurufu karatasi (printer) na nyaya zake zote vimeibwa mchana Agosti 5 mwaka huu na hadi sasa havijapatikana.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mganga Mkuu wa halmashauri hiyo, Mike Mabimbi amekiri kuibwa kwa mashine hiyo Agosti 5, 2019 mchana na bado haijapatikana.

Mabimbi amesema, baada ya kutokea kwa tukio hilo, walitoa taarifa jeshi la polisi, ambapo watu 17 wakiwemo wauguzi walikamatwa kwa ajili ya mahojiano.

Ni kweli mashine hiyo ambayo ilitolewa na wadau wa maendeleo UNFPA kwa ajili ya wodi ya akina mama tu, iliibiwa katika mazingira ya kutatanisha, tulishatoa taarifa polisi na wanaendelea na uchunguzi,” amesema Mabimbi.

Mganga huyo aliongeza kuwa mashine hiyo inafanana kama kompyuta mpakato, hivyo mtu yeyote mwenye nia ovu, alikuwa na uwezo wa kuiba na kuweka kwenye begi la mgongoni na kutoweka nayo.

Mashine hiyo ilitolewa kwa ajili ya akina mama wajawazito tu na ilikuwa kwenye wodi kwa ajili ya kurahisisha huduma, na wodi hiyo ilikuwa na vifaa vyote vinavyohitajika kwa mjamzito kikiwemo chumba cha upasuaji,” alisema Mabimbi.

Source: Habari Leo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents