Michezo

Masikini kocha wa Real Madrid!, wiki hii haiishi bila kutimuliwa nafasi yake kuchukuliwa na Mourinho

Rais wa klabu ya Real Madri, Florentino Perez huwenda akamtimua kazini meneja wa timu hiyo Julen Lopetegui siku ya Jumanne bila kujali matokeo yatakayopatikana kwenye mechi yao dhidi ya Viktoria Plzen hii ni kwa mujibu wa mtangazaji na mchambuzi wa habari za kiuchunguzi za michezo, Josep Pedrerol akiyasema hayo kupitia El Chiringuito.

Meneja wa timu hiyo Julen Lopetegui

🚨 information from ! “Lopetegui is going to sit on Tuesday in champions and everything seems to indicate that it will not in the Camp Nou.”

Pedrerol ambaye anaaminika kwa habari za kiuchunguzi amesema kuwa kocha Julen Lopetegui atatimuliwa kazi Jumanne na nafasi yake kurithiwa na Jose Mourinho kwakuwa ndiyo pendekezo la bodi ya klabu hiyo.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho

“Lopetegui ataifundisha Madrid hadi Jumanne na matokeo yoyote yatakayopatikana hayatamfanya asalie ndani ya Santiago Bernabeu. Mourinho ndiyo pendekezo la bodi ya klabu na wanafikiria kumuweka Solari hadi Mourinho atakapo kuwa huru kurejea Hispania. Solari atakuwa kocha wa muda tu,” amesema Pedrerol.

Hata hivyo Pedrerol ameongeza “Roberto Martinez ni  moja kati ya makocha wanao wania nafasi hiyo akiwemo Conte.”

Kwa mujibu wa El Chiringuito, Lopetegui hatakuwa kwenye mipango ya Real Madrid na huwenda akafika siku ya Jumapili baada ya El Clasico ambayo itaamua uwepo wake kama ataibuka na ushindi mbele ya Barcelona.

Kocha huyo wa kikosi cha Real Madrid B, Santiago Solari amesema kuwa yupo hapo kwaajili ya kuisaidia timu kutoka kwenye kipindi hiki kigumu.

⏳ Tic, TAC, TIC, TAC! ⏳”Real Madrid shuffles Solari as a PROVISIONAL technician and wait for Mourinho.” 🚨 the information in 🚨

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents