Michezo

Maskini Lukaku kuikosa Arsenal na Manchester derby (Picha)

Straika wa Manchester United, Romelu Lukaku huwenda akakabiliwa na adhabu ya kukosa michezo mitatu ya Ligi Kuu nchini Uingereza endapo atakutwa na kosa la kumchezea madhambi beki wa Brighton, Gaetan Bong katika mchezo wao siku ya Jumamosi.

Kipande cha ‘video’ kimeonyesha Lukaku akimpiga kwa kisigino mara mbili beki huyo wakati wa kupigwa kwa mpira wa kona katika lango la Brighton dakika chache kabla ya kupatikana kwa bao lililowafanya United kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

FA tayari wanafahamu tukio hilo wanachosubiri ni ripoti ya muamuzi wa mchezo huo, Neil Swarbrick kabla ya kutoa maamuzi.

United imetumia kiasi cha paundi milioni 75 kumsajili Lukaku  ambaye bilashaka endapo maamuzi yatatolewa ataikosa michezo mitatu dhidi ya Watford, Arsenal na wamwisho ni Manchester derby katika dimba la Old Trafford Desemba 10.

United itahitaji kuifunga City ili kuwa katika ushindani mzuri wa kuwania taji la EPL.

Mwezi uliyopita beki wa Liverpool, Dejan Lovren alimlalamikia Lukaku kwa kitendo cha kumpiga teke la uso hali iliyopelekea kupatikana bao lililopelekea mchezo huo kutoka sare katika dimba la Anfield huku FA ikishindwa kuchukua hatua juu ya malalamiko hayo.

Ingawa, Jose Mourinho ameshawahi kuzungumzia kumpumzisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ambaye amecheza kila dakika ambayo United imecheza katika ligi na klabu bingwa ila kupumzishwa na FA si vile alivyohitaji kocha huyo.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents