Technology

Mastaa wa Bongo wakesha live Instagram, saa chache baada ya huduma hiyo kuzinduliwa kwa wote

By  | 

Usiku wa Jumanne hii Instagram ilikumbwa na mafuriko ya live, saa chache baada ya huduma hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kuzinduliwa kwa watu wote.

Mastaa lukuki wa Bongo waliifakamia huduma hiyo na kuwa live kwa masaa kufurahia huduma hiyo. Wapo waliokuwa kitandani, wapo waliokuwa barabarani, wapo waliokuwa wakijifanyia interview wenyewe – kila mtu na eneo lake lakini walikuwa live.

Wengine walikesha wakiwa live, na wengine wameamka nayo asubuhi. Tangu ilipotangazwa November mwaka jana, huduma hiyo ilikuwa inapatikana katika sehemu chache tu duniani.

Baada ya Instagram live kukamilika, video hiyo haiwezi tena kupatikana na watumiaji, tofauti na huduma zingine ambapo video inaweza kuhifadhiwa na kutazamwa baadaye.

Instagram live videos zinaweza kutumia zaidi ya saa nzima.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments