AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Mastaa waendelea kumuombea bilionea Mo Dewji ikiwa ni saa 24 toka atekwe

Ni saa 24 toka bilionea kijana Mo Dewji atekwe na watu wasiojulikana Alhamisi hii akiwa GMY ya hotel ya Colosseum Oysterbay jijini Dar es salaam na mpaka muda huu hakuna taarifa mpya.

Kamanda Mambasasa amefunguka na kusema kuwa waliomteka ni wazungu wawili ambao bado hawajafahamika na dhumuni la utekeji bado halijajulikana ila jeshi la polisi limeanza ufuatiliaji wa tukio hilo.

”Niseme tu tukio hili limefanywa kwa kusimamiwa na wageni ambao ni wazungu wawili”.

Taarifa ya mwisho jana kutoka kwa kamanda huyo mapaka kufika majira ya jioni tayari jeshi hilo linawashikilia wa 12 kwaajili ya upelelezi wakiwemo walinzi ambao walikuwa wanalinda hotelini hapo.

Akizungumza jana na Clouds Fm, dereva huyo amesema kuwa ni jambo la kawaida kwa mfanyabiashara huyo tajiri kuendesha gari lake mwenyewe kwani alikuwa anaamini ana amani.

“Mo Dewji ni tajiri lakini anaishi maisha fulani hivi kama vile sio tajiri. Yaani alikuwa hana hofu na raia kwa sababu yeye kila mtu anayekutana naye ni kama vile anajuana naye miaka mingi,” alisema.

Dereva huyo ambaye amefanya kazi kwa Mo tangu mwaka 2001 ameeleza kuwa Mo alikuwa anajiamini na hakuwa na uoga dhidi ya raia, lakini aliwahi kumtahadharisha mwaka huu kuwa amekuwa akipokea jumbe za vitisho.

Hawa ni baadhi ya mastaa mbalimbali ambao bado wanaendelea kumuombea mfanyabishara huyo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW