Burudani

Mastaa waiunga mkono car wash ya Jaffarai

Ni saa kumi kasoro za jioni, jua la Dar es Salaam linawaka kama kawaida yake lakini haliwazuii wakazi wa jiji hili maarufu kwa foleni za magari kuendelea na shughuli zao. Wenye magari machafu yanayohitaji kuoshwa nao wanaelekea kwenye maeneo ya kuoshea magari ili kuyang’arisha.

Katika mitaa ya Mikocheni jirani kabisa na hospitali ya TMJ kwenye kituo cha mafuta cha Oil Com panakuwa kituo cha mwisho cha matembezi yetu. Tunapofika tunakaribishwa na mtu ambaye si mgeni katika macho yetu, Jaffarai. ‘Karibuni bana kwenye car wash yangu’ anatuambia Jafarai kwa uchangamfu mkubwa.

Pako busy mahali hapa. Kwa mbali tunaona magari kama matatu yakishughulikiwa na wafanyakazi wa car wash hii iliyozinduliwa rasmi leo (September 29). Tunakaa kwenye viti vizuri vilivyoandaliwa. ‘Kama unataka kinjwaji nini unaweza kujipatia hapa’ anasema Jaffarai.

Kwa mbali tunamuona msichana mmoja mrembo haswaaa! Kwa haraka haraka anaonekana ana miaka kama 19, 20 hivi. Huwezi kumwangalia mara moja ukatosheka, lazima urudie tena! Mwanzoni tunahisi pengine ni mteja pia, yaani kaleta gari lake. Hapana, huyu ni mfanyakazi wa Car Wash hii ya Jafarai. Kazi yake ni moja tu, kukaribisha wateja wanaoleta magari yao. Kazi anaiweza. Tabasamu lake tu linaweza kuifanya siku yako iwe tamuuuu kwelikweli!

Wakati tunakaa na kujaribu kuhamisha akili zetu kutoka kwa mrembo huyo, tunamwona karibu yetu mtangazaji wa Clouds FM, Reuben Ndege aka Nchakali, Dj na blogger maarufu jijini Dar es Salaam Dj Choka wakiwa ni miongoni mwa watu waliopo hapa.

Nchakali kaja kumuunga mkono Jaffarai kwa kuleta gari yake kuoshwa. Lakini Dj Choka lengo lake na sisi ni moja, picha na habari. Nchakali anasikika akimpa ushauri Jafarai kuwa aweke screen kubwa ili mashabiki wa mpira kama yeye waweze kufurahia na pia aweke wireless internet ili wateja wabrowse internet wakati wakisubiri magari yao. Jafarai anaahidi kuyafanyia kazi maoni hayo.

Wakati tunaendelea kuangalia nani yupo hapa, kwa mbali inaingia gari nyeupe ndogo ikiwa na muziki mzito wa Chris Brown. Mara anashuka TID aka mnyama!! Anaonekana kuwa ameshakuja awali kwakuwa alifika na kuendelea na story za watu waliofika hapa.

Anaanza kutoa story za muziki wa Marekani na mambo mengine. Baada ya kusoma mazingira tunamuita Jaffarai pembeni ili tuzungumze mawili matatu kuhusiana na uzinduzi wa kituo chake cha kuoshea magari. Kabla maongezi yetu hayajanoga vizuri mara inaingia Prado nyekundu na inapita karibu yetu kiasi cha kuyapeleka macho yetu kule na kupoteza concentration yetu kwa muda.

Anashuka supastaa mwingine. Huyu ni Lamar, producer wa Fish Crub. Anataka kuja tulipo kwa lengo la kuongea na Jafarai lakini anagundua kuwa tuna maongezi muhimu tunayoendelea kuyafanya.

Swali la kwanza kwa Jaffarai ni kuhusu umri wake leo katika siku yake ya kuzaliwa na kwanini ameamua kuzindua Car wash yake siku hii:

“Namshukuru mwenyezi Mungu nina miaka mingi ndio maana nafikiria sasa hivi kwakuwa umri umeenda nataka pia kipato kiende huwezi kuona umri unaenda halafu kipato kiko pale pale ndio maana nimeamua kufungua car wash kwasababu naangalia kitu tofauti kwasababu, nimefanya muziki kwa miaka kumi lakini nikaona kwamba nahitaji kitu kingine mbadala nje ya muziki kwasababu biashara ya muziki kama unavyoijua kuna sehemu unapanda kuna sehemu unashuka, kwahiyo nahitaji kuwa na biashara nyingine zaidi ya muziki ili kipush maisha yawe yanaenda,” anasema Jaffarai.

“Nilikuwa nizindue kama wiki mbili zilizopita nikasema acha nisubiri siku ya birthday yangu kwasababu hii inanipa motisha fulani sababu naona mwaka huu ambao ninauanza leo majukumu yanaongezeka hivyo inabidi niwe serious na vitu vingine nje ya muziki. Plan ya kuanzisha car wash ni kwasababu nimeona ninataka kufanya biashara nyingine tofauti kidogo, sitaki kufanya biashara inayofanywa na watu wengine. Pia tuna uhaba wa car wash Dar es Salaam na magari yako mengi sana kama unavyojua, kila mtu ana gari siku hapa mjini unajua, car wash ziko chache halafu nyingi ziko local. Car wash ya kisasa kama hii hapa ni chache.”

Katika maongezi yetu anagusia pia mipango ya kuongeza matawi mengine ya car wash yake jijini kadri Mungu atakavyomjalia lakini anasema kuwa muziki bado ataendelea kufanya sababu ndio uliomfikisha hapo alipo.

“Muziki siwezi kuacha, muziki ndio maisha bila muziki hata hii car wash isingekuwepo. Kuna watu wazima mpaka leo wanaimba, kwahiyo nitaimba mpaka nitakapokufa.”

Jaffarai hakuacha kuwapa ushauri wasanii wengine wakongwe ambao maisha yamekuwa magumu na kubakia kulalamika kila siku. “Kubwa zaidi ni kujipanga kwasababu, tusijisahau sababu maisha ya ustaa ni maisha fulani ya kupita, hauwezi kuwa staa forever, tumeshasikia mastaa kibao walikuwa juu sasa hivi wameshuka. Kwahivyo wasanii wenzangu wajaribu tu kuinvest pembeni ya muziki yaani. Haya maisha ni magumu kama wewe mwenyewe ukifanya yawe magumu lakini maisha sio magumu ukifanya yasiwe magumu. Watu wanatakiwa wajitume, unajua biashara ni kujaribu, Mungu mwenyewe anakuambia jaribu utapata, umejaribu mara ngapi? Hujajaribu hata mara moja unalalamika, jaribu kwanza ukishindwa kitu ndio uanze kulalamika kweli maisha magumu lakini jaribu kwanza.”

Baada ya mahojiano hayo na Jaffarai tunarudi katika siti zetu na kuanza kuangalia kinachoendelea. Muda mfupi anaingia staa mwingine. Huyu ni msanii wa Hip Hop ambaye hujihusisha pia na boxing, Zola D. Anaingia na ‘mdoli’ mwekundu na kabla hajashuka, msichana mrembo tuliyemzungumzia mwanzo anamfuata na kumkaribisha kwa tabasamu tamu kama kawaida yake. Zola anajumuika na list ya mastaa kibao waliokuja kumpa support Jafarai.
Car wash inaendelea kuchangamka na story zinanoga. Huu umekuwa mwanzo mzuri kwa Jafarai.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents