Habari

Mastaa wamlilia director aliyejitupa chini ya daraja

Mastaa wa filamu nchini Marekani wameendelea kuonesha kusikitishwa kwao na kifo cha director wa filamu maarufu nchini humo Tony Scott. Scott alijiua juzi Jumapili kwa kujitupa chini ya daraja la Vincent Thomas jijini San Pedro, California.
Alikuwa na umri wa miaka 68.

Marc Anthony ambaye aliigiza kwenye filamu iliyoongozwa na Scott, ‘Man on Fire’ ameutumia mtandao wa Twitter kuelezea masikitiko yake kuhusiana na habari hizo za kushtusha: “Rest in peace, brother. Tony Scott, a genius silenced. I am devastated!! Why?????”

Muigizaji Rosario Dawson, ambaye aliigiza kwenye filamu ya mwaka 2010 aliyoongoza Scott ya Unstoppable, aliandika: “Tony Scott … you left us too soon. How terribly sad. What a lovely, kind human being you were. I will love and miss you much.
Blessings to your family. Rest in peace.”

Wengine walioandika ni pamoja na muimbaji Justin Timberlake aliyesema: “So sad to hear the news about Tony Scott. His movies made growing up more fun for me. My prayers and condolences to the Scott family.”

Mwingine aliyeumizwa zaidi na kifo hicho ni Tom Cruise ambaye alimchukulia Scott kama mtu aliyemsaidia kuwa nyota mkubwa wa Hollywood.

Tony Scott, aliongoza filamu ya Cruise ya mwaka 1986 Top Gun na ya mwaka 1990 Days of Thunder. Jana Cruise aliandika maelezo yasemayo: “Tony was my dear friend and I will really miss him. He was a creative visionary whose mark on film is immeasurable. My deepest sorrow and thoughts are with his family at this time.”

Mwili wa Scott uliopolewa nje ya maji na polisi wa Los Angeles, LAPD, wakati wa doria.
Mashuhuda walidai kuwa hakusita kujirusha chini ya daraja hilo.
Ameacha mke Donna Wilson Scott, na watoto wawili Frank na Max.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents