Michezo

Mastaa wazungumzia Taifa Stars kufungwa 7-0 na Algeria

Baada ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kutupwa nje ya mbio za kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi kwa aibu kubwa ya mabao 7-0 kutoka kwa Algeria, mastaa na wadau mbalimbali wa michezo wametoa maoni yao.

????????????????????????????????????

Kupitia kurasa za kijamii haya ni maoni yao:

Ridhiwani Kikwete

That Moment we realise that we wasted Five Open chances to Score on our first Leg , Is when we found

JB

Hakuna maajabu kwenye mpira..kama unajua unajua tu…tusiwalaumu..tutengeneze timu…tena tuanze na vilabu vyetu..wenye pesa waachwe wawekeze…hakuna short cut.

H Baba

Timu yetu kufungwa sishangai #watanzania tunaipenda timu yetu ila #WAULIZENI TFF kipato kilichopatikana mechi ya taifa wachezaji walipewa bei gani? Unaweza kukuta posho yakila mchezaji kapewa laki 2 wakati pesa zimeingia kibao WANAKULA WAO nyie mnalaumu nachojua team yetu ya #taifa wanafaidika wengine kabisa sio wachezaji wetu #wachezaji wanatakiwa kupewa nguvu kwa ahadi nzuri tuu ili wacheze kufa nakupona #mchezaji acheze kufa nakupona anaekula mwingine wachezaji wanaumia wao nalawama wao pia #Walaji wengine ata kama nimimi sichezi kwa nguvu #poleni wachezaji wetu wa #tz mnawashibisha watu.

MwanaFA
Algeria kwa niaba ya wote tunakuomba msamaha, samahani sana tumekoma na hakya Mungu haturudii tena kukuchokoza!

Zitto Kabwe

Brazil walifungwa 7 sembuse Tanzania? Muhimu kujifunza na kujipanga upya…… tuwekeze kuendeleza vipaji na kujenga timu. Inawezekana. Ethiopia si walikuwa kama sisi bana.

Mbwana Samata

Matokeo yalikuwa mabaya sana, wote yametuumiza, na inauma sana unapokuwa uwanjani ukijitahidi kufanya kila liwezekanalo lakini mambo hayaendi sawa na huku ukijua kuna mamilioni ya watu wanaotumaini mazuri yafanyike na wanatoa sapoti yao. kushindwa michuano ni sawa na unaposhindwa vita, unaweza ukaamua kukata tamaa kabisa na kufia uwanja wa mapanbano, au unaweza kukubali kushindwa kabla matumaini hayajafa ukaretreat ili ujipange upya. mimi naiamini option ya pili. ndio option ambayo inafanya ndoto ziendelee kuishi na maisha yaendelee. ninameza maumivu na kuendelea na safari japo hayatokata kiu, ila muhimu ni kupita kwenye kipindi kigumu kama hiki. kushindwa sio silaha ya kutokomeza imani, ila ni teke linalompa maumivu chura na kumfanya atafute njia nyingine ya kupita mpk afike safari yake. ‪#‎Proudly_Tanzanian‬

From The Desk Of Shaffih Dauda

Moja kati ya matatizo makubwa ya sisi watanzania ni kutokukubali pale ambapo kuna mtu amekuzidi. Mara nyingi huwa tunadharau yule ana nini, mfano mtu ana gali zuri watasema yule kahongwa au kaiba. Hatukubali uhalisia au mafanikio ya mtu ili kujipa changamoto angalau kama sikufikia au kukaribia mafanikio ya aliyekutangulia.

Maana yake ni kwamba zile jitihada za uhongo zilizokua zifanywa na TFF kuwaaminisha watanzania kwamba tunaweza kuifunga Algeria kitu ambacho ni cha uongo kabisa. Ndio maana mimi toka mwanzoni nilikua napinga kwa asilimia zaidi ya 100 kuhusu swala la kuifunga Algeria. Ndio maana tangu mwanzoni nilitoa ahadi kwamba kama Algeria ikitolewa na Tanzania basi nitaenda gerezani, napapenda uraiani ndio maana nilikua na uhakika hilo swala lisingewezekana.

Mpira hauna short cut ni mipango ambayo ipo clear, TFF ilicheza na saikolojia ya watu baada ya wao kushindwa kazi yao ya msingi kusimamia uwekezaji wa soccer. Waliwadharau Algeria, wakaunda kamati ambazo ilikuwa ni njia ya kuwaada na kuwaaminisha watanzania kwamba inawezekana kirahisi kuwafunga Algeria.

Sifurahii matokeo lakini kwa upande mwingine nafurahia. Hii iwe fundisho kwa viongozi ambao wana mentality za kishabiki badala ya kusimamia na kutengeneza misingi thabiti ya kuendeleza soccer letu, wanabaki kuendeleza propaganda za kuwarubuni watanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents