Burudani

Master J asema tuzo za kimataifa wanazopata wasanii wa Tanzania haziwanufaishi

Mtayarishaji mkongwe wa muziki na jaji wa mashindano ya Bongo Star Search, Master Jay, amesema tuzo wanazoshiriki wasanii wa Tanzania nje ya nchi haziwasaidii katika kutanua wigo wa kibiashara wa msanii hao.

MasterJ

Akizungumza na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Master Jay alisema wasanii wa Tanzania wamekuwa wakitumia gharama kubwa kutengeneza video zenye ubora ili kujitangaza lakini manufaa yamekuwa madogo.

“Kusema kweli sijaona inatusaidia nini, ukiniuliza mimi mtu wa label, unafanya video kali ili ipigwe kwenye station za nje za televisheni ili upanue soko, hilo ndio lengo kuu kwamba tayari sawa nimeshaweka such record hapa Tanzania Mungu kanibariki, Je, nitaingiaje Mozambique, Zambia, Zimbabwe na kadhalika? Naona video zinafanyika wanaalikwa kwenye tuzo, lakini sioni mtu akiwa anafanya show tofauti na zile alizokuwa akizifanya kabla,” alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents