Burudani
Master P aachia ngoma maalum kwa ajili ya siku ya akina Mama Duniani ‘Mother’s Day’
Katika kusherehekea siku ya akina Mama Duniani leo Muigizaji na Rapa Maarufu kutoka Marekani Master P ameachia wimbo mpya kama zawadi kwa Mama yake na akina mama wote ulimwenguni.
Mmiliki huyo wa Lebo ya ‘No limit Records’ ameamua kutunga wimbo huo wa ‘Love you Momma’ akishirikiana na mtoto wake Romeo, kama Dedication kwa Mama yake mzazi na wazazi wengine Duniani kote.
Usikilize wimbo huo hapa chini
Siku ya akina Mama Duniani hufanyika kila Jumapili ya pili ya Mwezi May kila mwaka na kwa mara ya kwanza ilianzia nchini Marekani mnamo Karne ya 20.
By Godfrey Mgallah