Habari

Mataifa 6 ya EU kujadili mustakabali wao baada ya Uingereza kujiondoa

Mataifa 6 waanzilishi wa Muungano wa Ulaya EU wanakutana leo kujadili mustakabali wao wa baadaye baada ya Uingereza kuamua kujiondoa kutoka kwa muungano huo.

141218194255_eu_summit_brussels_640x360_getty_nocredit
EU

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, ufaransa,Italy, Ubelgiji, Luxembourg na Uholanzi wanatarajiwa kuanzisha mchakato huo pasi na kuwa na ngoja ngoja.

Tayari rais wa tume ya muungano wa Ulaya , Jean-Claude Juncker, amesema anataka kuanzisha majadiliano mara moja ya jinsi Uingereza itakavyotoka rasmi kutoka EU.

160318162042_turkey_greece_eu_640x360_ap_nocredit
Baadhi ya Viongozi wa Muungano wa Ulaya

Bw.Juncker amesema haieleweki kwamba swala hilo likumbwe na hadi waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, ang’atuke kutoka madarakani baada ya kushindwa katika kura hiyo ya maoni iliyoamua nchi hiyo ijibandue kutoka Umoja wa Ulaya.

Mawaziri hao pia wanatarajiwa kuweka masharti mapya yatakayowazuia wanachama wengine kuiga mfano wa Uingereza,baada ya vyama vya mrengo wa kulia katika mataifa mengi duniani kupongeza uamuzi huo wa Uingereza kujitoa kutoka muungano wa Ulaya.

Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, amewatahadharisha wenzake kutokuwa na hamaki na kutaka kuchukua hatua za kama kuilipizia kisasi Uingereza .

Ameomba kuwepo kwa subra na umakini katika kulishughulikia swala hilo ambalo anasema linapaswa kuongozwa tu na vipi kushughulikia mahitaji ya raia wa jumuiya ya muungano wa Ulaya.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents