Technology

Mataifa 99 yaathiriwa na uhalifu wa mitandaoni

Kampuni ya kulinda uhalifu wa mitandao Avast, imesema kuwa imeona kesi 75,000 za programu zinazotumika kufanya uhalifu mtandaoni inayojulikana kama ‘WannaCry’ duniani.

Shambulizi la kihalifu kupitia mitandao yanatendeka kupitia vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti duniani.Kuna ripoti za mashambulizi katika mataifa 99 ikiwemo Urusi nchini China.

Kati ya mashirika yalioathirika zaidi ni shirika la huduma za afya nchini Uingereza na “Uskochi”,Idadi kubwa ya kampuni kubwa ikiwemo Telefonica ,kampuni ya umeme ya Iberdrola na ile ya Gesi asilia pia ziliathirika huku ripoti ikisema kwamba wafanyikazi katika kampuni hizo waliagizwa kuzima kompyuta zao.

Programu hiyo ilisambaa siku ya Ijumaa ambapo ilitaka malipo ya dola 300 ilikufungua faili ilizokuwa imeziteka nyara muhimu katika kompyuta.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents