Habari

Matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018 yatangazwa, Arusha na Dar zafunika kwenye Top 10 ya shule zilizofanya vizuri kitaifa

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) leo Alhamisi Julai 11, 2019 limetangaza matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2018.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA mjini Unguja Zanzibar, Dkt. Charles Msonde amesema ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 98.32 mwaka 2019 ikiwa ni sawa ongezeko la 0.74% .

Matokeo ya mtihani huo uliofanywa Mei 6 hadi 23 mwaka huu, Ulifanywa na watahiniwa 91,298 wasichana 37,948 sawa na asilimia 41.56 na wavulana 53,350 sawa na asilimia 58.44.

Dkt. Msonde amesema kati ya watahiniwa 91,298 waliosajiliwa kufanya mtihani huo, watahiniwa 90,001 sawa na asilimia 98.58 walifanya mtihani na watahiniwa 1,297 sawa na asilimia 1.42 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ugonjwa na utoro.

Akitaja shule 10 zilizofanya vizuri, Dk Charles Msonde amesema shule iliyoshika nafasi ya kwanza ni Kisimiri ya mkoani Arusha iliyokuwa na watahiniwa 60.

Feza Boys ya Jijini Dar es Salaam yenye watahiniwa 87 imeshika nafasi ya pili ikifuatiwa na Ahmes ya mkoani Pwani iliyokuwa na watahiniwa 112.

Mwandet yenye watahiniwa 77 ya mkoani Arusha imeshika nafasi ya nne huku Tabora Boys ya mkoani Tabora yenye watahiniwa 109 imeshika nafasi ya tano.

Kibaha ya mkoani Pwani yenye watahiniwa 172 imeshika nafasi ya sita na kufuatiwa na Feza Girls (watahiniwa 66), St Mary’s Mazinde Juu (216), Canossa (83) na Kemebos (33).

Tazama matokeo kwenye link – MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2019.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents