Michezo

Matokeo ya Ligi Kuu nchini Uingereza

Michezo mbalimbali imepigwa Jumamosi ya leo katika Ligi Kuu nchini Uingereza, Manchester United ikiwa nyumbani Old Trafford imechomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Brighton lililofungwa na Lewis Dunk dakika ya 66 ya mchezo.

Kwa matokeo hayo sasa United yenye pointi 29 inaachwa nyuma kwa alama tano mbele ya vinara waligi timu ya Manchester City wenye pointi 34.

Crystal Palace ikiwa nyumbani huko Selhurst Park imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Stoke City.

Wakati Newcastle ikiwa nyumbani imepokea kipigo cha mabao 0-3 dhidi ya Watford huku Swansea ikitoka sare tasa ya bila kufungana nyumbani dhidi ya Bournemouth na Tottenham ikitoka sare ya bao 1-1 mbele ya West Brom wakati Spurs ikisawazisha bao hilo dakika ya 74 kupitia kwa Harry Kane.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents