Michezo

Matokeo ya mechi za robo fainali ya Europa ligi

Michuano ya robo fainali ya Europa ligi imechezwa katika viwanja vinne tofauti kwa michezo minne.

Liverpool wakiwa ugenini nchini Ujerumani walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Borrusia Dortmund, Divock Origi aliwafungia Liverpool bao la kuongoza kabla ya beki wa Dortmund Mats Hummels kusawazisha.

32F2550F00000578-0-image-a-2_1460058913614

Sevilla wakawachapa ndugu zao wa Athletic Bilbao kwa mabao 2-1mabao ya ushindi ya Sevilla yakifungwa na Timothee Kolodziejczak na Vicente Iborra, huku bao la kufutia machozi la Bilbao likifungwa na Aduriz Zubeldia.

32F28D0000000578-3528912-image-a-64_1460062484661

Sporting Braga wakiwa wenyeji wa Shakhtar Donetsk walikubali kulala kwa kichapo cha mabao 2-1,wachezaji Yaloslav Rakitskiy na Facundo Ferreyra wakifunga mabao ya ushindi, huku Naval Costa Eduardo kwa Braga.

Villarreal wakicheza katika dimba la El Madrigal wlichomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sparta Prague, Cedric Bakambu akifunga mabao yote mawili kwa upande Villareal huku Jakub Brabec akifunga bao pekee la Sparta

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents