Michezo

Matokeo ya michezo mbalimbali barani Ulaya

Michezo kadhaa imechezwa hapo jana barani Ulaya ambapo nchini Hispania, mabingwa klabu bingwa barani Ulaya na La Liga, Real Madrid ilichomoza na ushindi wa jumla ya mabao 3-0 mbele ya timu ya Deportivo.

Mabao ya Madrid yakiwekwa kimyani na (Bale  dakika ya 20, Casemiro  27 na Kroos  mnamo  dakika ya 61 kipindi cha pili).

Wakati kipa wa Real akifanya kazi kubwa ya kuokoa mchomo wa penati dakika ya 88 timu hiyo ikajikuta inapoteza mchezaji wapili muhimu kwa Ramos kupewa kadi nyekundu dakika za lala kwa buriani na hivyo kuungana na Cristiano Ronaldo katika kukosa baadhi ya michezo inayofuata.

Mahasimu wao Barcelona nao wakichomoza na ushindi mwembamba wa mbao 2-0 dhidi ya Real Betis.

Barca ambayo inaonekana kuyumba baada ya kukosa huduma ya mbrazili Neymar ambaye ameuzwa kwa rekodi ya dunia ya paundi milioni 222 kwenda PSG huku mchezaji wao wa kimataifa wa Uruguay, Luis Alberto Suarez Diaz akiwa anasumbuliwa na majeruhi ilipata mabao yake kupitia kwa  (Tosc dakika ya 37, na Roberto dakika ya 39) ambapo goli hilo la kwanza beki wa Betis alijifunga.

Barcelona wameingia dimbani wakiwa na jezi zisizo na majina kama sehemu ya kuomboleza vifo vilivyotokana na shambulio la kigaidi lililolikumba Jiji la Barcelona wiki hii.

Bado kuna utata juu ya mfungaji wa bao la kwanza la Barca. Wachezaji watatu wamehusika Messi, Deulefeu, na beki wa Betis, Tosc

Na huko League1 nchini Ufaransa matajiri wa jiji hilo klabu ya Paris Saint-Germain imechomoza na ushindi mnono wa jumla ya mabao 6- 2 dhidi ya Toulouse.

Tokeo la picha la PSG 6-2

Mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa raia wa Brazili, Neymar amezidi kuonyesha chechezake katika ligi hiyo baada ya kutumbukiza kimyani mabao mawili kati ya sita yaliyofungwa na timu yake ya PSG.

Wafungaji wa mchezo huo (Neymar dakika ya 31 na 90, wakati  Rabiot akifunga dakika ya 35, Cavan 75, Pastore 82, Kurzawa 84  huku mabao ya kufutia machozi ya Toulouse yakifungwa na Gradel dakika ya 18 mchezaji Jullien akifunga kunako dakika ya 78)

Tokeo la picha la PSG 6-2

Huko nchini Uingereza  Klabu ya Meneja wa Chelsea, Antonio Conte ikichomoza na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Tottenham Hotspurs.

Tokeo la picha la tHE bLUES 2-1 Spurs

Shujaaa wa The Blues hapo jana ni mchezaji, Marcos Alonso aliyefunga mabao mawili katika dakika ya 24 na 88 ya mchezo wakati Spurs ikipata bao lake kupitia kwa Batshuayi.

Wakati klabu ya Huddersfield ikifanikiwa kushinda mchezo wake wapili wa Premier League huku mchezaji, Aaron Mooy akiifungia bao moja na la ushindi dakika ya 50 ya kipindi cha pili dhidi ya Newcastle.

Mooy, mwenye umri wa miaka 26, ambaye ni kiungo kutoka Sydney ameonekana kufanya vizuri zaidi msimu huu na kujihakikishia maisha katika kikosi cha Huddersfield.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents