Michezo

Matokeo ya michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom

Michezo kadhaa imechezwa hii leo ya duru ya tatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika viwanja mbalimbali hapa nchini.

Huko Majimaji mjini Songea mwenyeji Majimaji FC imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga SC, Mtibwa Sugar ikiwa nyumbani imechomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC, Tanzania Prisons ikitoka sare ya bila kufungana wakiwa nyumbani dhidi ya Ndanda FC, wakati Lipuli ikitoka sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting na klabu ya Stand United ikikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Singida.

Hapo kesho mzunguko huo wa tatu utakamilishwa kwa wapenzi wa soka kushuhudia michezo miwili ambapo Simba SC kiwa nyumbani katika dimba la Uwanja wa Uhuru itawakabili  Mwadui FC  ilhali Mbeya City ikiwakaribisha timu ya Njombe Mji katika dimba la Sokoine.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents