Matonya atoroka Jela

Ombaomba mkongwe na maarufu nchini, Anthony Matonya ametoroka kwenye kambini alikokuwa akitumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja kwa kosa la uzururaji na kuomba fedha bila sababu za msingi.

matonya_1.jpg

 

Ombaomba mkongwe na maarufu nchini, Anthony Matonya ametoroka kwenye kambini alikokuwa akitumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja kwa kosa la uzururaji na kuomba fedha bila sababu za msingi.

Matonya ambaye awali alikuwa jijini Dar es salaam akiomba mitaani alihamia Morogoro baada ya kutimuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusufu Makamba, ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kurudishwa kwao Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, alisema hatua kali yake kutokana na kitendo chake cha kutoroka na kurudi mitaani mjini Morogora kuendelea na uzururaji.

Akizungumza na mwandishi, Mwambungu alisema kitendo cha Matonya kutoroka katika kambi ya Kulelea Wazee wasiojiweza ya Fungafunga pamoja na kabla ya kumaliza adhabu aliyopewa na Mahakama ya Mwanzo ya Nunge Mei, mwaka huu ni kosa kwa mujibu wa sheria, hivyo ni lazima akamatwe na kufikishwa tena mahakamani.

Mwambungu alisema kampeni ya kumsakama ombaomba huyo na wenzake itafanyika mwishoni mwa wiki na kukakikisha kwamba anakamatwa na kurudishwa kwenye kambi hiyo na kufikisha mahakamani kwa kosa la kutoroka akiwa chini kifungo.

Alifahamisha kuwa atakapomaliza kifungo atarudishwa kijijini kwao mkoani Dodoma, chini ya ulinzi wa polisi. ”Matonya na wenzake wamegeuka kero kwa wakazi wa Halmshauri ya Morogoro kwa kosa la kuzurura kwenye nyumba za starehe, hotelini, ofisi za serikali, kwenye mitaa ya katikati ya mji, mikusanyiko ya watu na madukani kuombaomba,” alisema Mwambungu na kuongeza: ”Asilimia kubwa ya ombaomba hao ni watu wenye viungo kamili na wenye nguvu za kufanya kazi za kujipatia riziki zao, lakini wamekuwa wakizurura mitaani kuomba fedha kwa kisingizo cha kwamba hawana uwezo”.

Alisisitiza kuwa, kitendo cha Matonya na wenzake kukiuka amri ya serikali ya kuzurura ovyo na kuomba omba fedha mitaani ni cha aibu, hivyo ni lazima kikomeshwe ili kuwadhibiti watu wengine wa aina hiyo kuingia mjini Morogoro kutoka mikoa mingine.

Baaada ya Mkuu wa Wilaya kutoa madai hayo, mwandishi wa habari hizi, alimsaka Matonya na kukuta kwenye eneo la daraja la Shani akiomba fedha kwa wapita njia.

Alipomuuliza sababu za kutoroka katika kambi ya Fungafunga alikokuwa kifungoni alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na kukosekana huduma muhimu za kibinadamu kambini hapo.

Alisema hawezi kuishi kwenye kambi hiyo kwa sababu hana fedha za kununulia sabuni, mafuta ya kupakaa na mahitaji mengine muhimu na kwamba ndio maana aliamua kutoroka na kurejea tena mitaani ambako hujipatia riziki kwa kuombaomba.

”Kamwe sirudi kambini na wala huko kijiji kwa sababu sina mtu wa kunihudumia zaidi ya mjini ambako naomba na kupata fedha za kujikimu,” alisema Matonya.

Kwa sasa Matonya anafanya shughuli za kuomba fedha katika eneo la daraja la Shani, barabara Stesheni kisha huenda katika hoteli ya Yemen iliyopo katikati ya mji ambako hunywa chai na kupata chakula cha mchana na usiku, kisha kwenda kulala stesheni.

Baada ya Mahakama kumhukumu Matonya kifungo hicho, Idara ya Ustawi wa Jamii ya Mkoa wa Morogoro, ilimuamuru atumikie kifungo hicho kwa kambi hiyo na atakapomaliza arejeshwe kwao Dodoma.

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents