Burudani

Matonya: Sasa hivi kila mwezi na ngoma mpya

Matonya hataki tena kukaa kimya muda mrefu bila kuachia wimbo mpya. Sasa amepanga kuachia ngoma kila mwezi.

10932622_1397002317274040_2122099994_n

Akiongea na E-News ya EATV msanii huyo amesema amesikia kilio cha mashabiki wake kuwa wanamiss kazi zake.

“Sasa hivi nipo kikazi zaidi, mwanzo nilikuwa nimetingwa na majukumu binafsi na shughuli za hapa na pale,” alisema.

“Nashukuru sasa hivi majukumu yamekaa vizuri, kwahiyo sasa hivi nipo kikazi zaidi. Nawakaribisha wote ambao wanataka kushirikiana na mimi kikazi. Na pia sasa hivi itakuwa ni bandika bandua, yaani nitakuwa natoa ngoma kila mwezi maana nasikia mashabiki wangu mtaani wamenimiss sana.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents