Matukio makubwa ya Maradona ndani na nje ya uwanja

Matukio ya Maradona

  • 1977: Alijitokeza katika mchuano kati ya Argentina v Hungary
  • 1982: Alijiunga na Napoli baada ya kuwa Barcelona kwa miaka miwili ya mafanikio makubwa
  • 1986: Alishinda Kombe la Dunia akichezea Argentina
  • 1990: Alikuwa mshindi wa pili wa Kombe la Dunia akichezea Argentina. Kombe la pili la Ligi Napoli
  • 1991: Alipigwa marufuku ya miezi 15 baada ya kuthibitishwa kutumia dawa zilizopigwa marufuku
  • 1994: Alicheza katika kombe la dunia kwa mara ya nne lakini akatolewa nje baada ya kuthibitishwa kutumia dawa zilizopigwa marufuku
  • 1997: Alistaafu kucheza soka baada ya kuthibitishwa kutumia dawa zilizopigwa marufuku kwa mara ya tatu
  • 2010: Alikamilisha miaka miwili ya kuwa kocha wa Argentina baada ya kutolewa katika robo fainali ya Kombe la Dunia

Maisha baada ya kustaafu

Baada ya kupatikana tena ametumia dawa zilizopigwa marufuku, miaka mitatu baadaye alistaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 37 lakini akaendelea kuandamwa na matatizo.

Maradona alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na miezi 10 kilichocheleweshwa kwasababu ya kufyatulia risasi wanahabari hewani .

Tabia yake ya kutumia dawa za kulevya na pombe ilimsababishia matatizo mengi ya kiafya. Aliongeza uzito na kuna wakati fulani alikuwa na kilogramu 128. Mwaka 2004 akapata mshtuko wa moyo uliosababisha apelekwe katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Pia alifanyiwa upasuaji wa kupunguza tumbo lake kumsadia kukabiliana na tatizo la uzito wa kupindukia na kutafuta hifadhi Cuba wakati anakabiliana na utumiaji wa dawa za kulevya.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW