Michezo

Matumaini ya kumpata mchezaji wa Cardiff aliyepotea angani na Ndege yafifia, Afisa wa mambo ya anga aeleza hali ilivyo

Hakuna matumaini ya kumpata mchezaji wa Cardiff City, Emiliano Sala, amesema mmoja wa maafisa wa uokozi.

Mshambuliaji huyo raia wa Argentina,mwenye umri wa miaka 28, na rubani walikua wameabiri ndege iliyopotea katika viswa vya Channel Jumatatu usiku.

Kwa mujibu wa BBC, Afisaa mkuu wa visiwa vya Channel anayesimamimia shughuli ya kutafuta ndege, John Fitzgerald, amesema “hata mtu aliye na afya nzuri zaidi” hawezi kupona akiwa ndani ya maji kwa saa kadhaa.‘Hakuna matumaini’ ya kumpata nyota wa soka

Shughuli ya kutafuta ndege hiyo iliyopotea na abiaria waliyokua ndani iliripotiwa siku ya Jumatano.

Sala aliripotiwa kutuma ujumbe wa sauti kwa mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwa familia yake akisema “naogopa sana”.

Vyombo vya habari nchini Argentina vimeripoti kuwa alisema: “Nimepanda ndege ambayo inaonekana kama ina hitilafu itaanguka.”

Ilipofika saa za mchana siku ya Jumatano, idara ya Polisi ya Guernsey ilisema kuna ndege tatu na helikopta moja angani huku wakijaribu kutafuta uwezekano wa kupatikana kwa ndege ya Piper Malibu.


Mashabiki wameweka mashada ya maua nje ya uwanja wa Cardiff City

Vikosi pia vilisema “vinachunguza picha za satellite na data ya simu kubaini ikiwa zinaweza kusaidia katika shughuli ya kuitafuta ndege hiyo. Kufikia sasa hatujapata chochote kinachoashiria ndege iliyopotea”.

Sala alikua safarini kuelekea mji wa Welsh baada ya kutia saini mkataba wa pauni milioni 15 kujiunga na Bluebirds kutoka klabu ya Nantes ya Ufarasa.

Bw.Fitzgerald amesema: ” Nasikitika kwasababu sidhani kama kuna matumaini yoyote. Wakati huu wa mwaka hali ya hewa ni mbaya sana kuwa ndani ya maji ni hatari zaidi.”

Polisi ya Guernsey wana tathmini vitu vinne ambavyo huenda vimekumba ndege hiyo ikiwa ni pamoja na kama ndege ilianguka majini, na kuwaacha majini” ama “walitua majini na wanamatumaini ya kuokolewa kutoa kwa ndege yenyewe”.

“kile tunachopatia umuhimu ni uokozi,” ilisema kikoso cha uokozi

Huku hayo yakijiri mwnyekiti wa, Cardiff City Mehmet Dalman amesema hakuna mpango wa kubadilisha kikosi kitakachoshiriki ligi ya kuu ya England dhidi ya Arsenal katika uwanja wa at Emirates Januari 29.

Bw. Dalman amesema wachezaji na mashabiki wamesikitishwa sana na tukio hilo na kwamba klabu imepokea ujumbe wa pole kutoka kila pembe duniani.


Mashabiki wa Nantes wamekusanyika mjini humo kutoa heshima zao kwa mshambuliaji wao wa zamani

“Familia ya kandanda ina njia ya kipekee ya kuja pamoja wakati wa majanga,” Aliiambia kituo cha BBC Radio Wales.

Pia alithibitisha kuwa klabu haikuhusika na usafari ya Sala katika ndege hiyo”.

“Tutafanya kila juhudi kuhakikisha ukweli kuhusiana na mkasa huo unajuklikana,” aliongeza Bw. Dalman.

Vikosi vya uokozi Angani na majini kutoka visiwa vya Channel, Ufaransa na Uingereza vilishirikikatika oparesheni ya kutafuta ndege hiyo kwa saa 15 siku ya Jumanne lakini hawakufanikiwa kuipata ndege hiyo na abiria wake.

Baba yake Sala, Horacio ameiambia chombo kimoja cha habari nchini Argentina kuwa: “Kila muda unavyosonga ndivyo nashikwa na hofu.

“Natumai watampata. Mara ya mwisho walisema kuwa mawasiliano yalikatika walipovuka mto[English Channel].”


Sala alifungia Nantes mabao 48 alipojiunga nayo 2015

Usiku wa kuamkia leo mashabiki wa kandanda mjini Nantes waliweka mashada ya maua kwa heshima ya Sala na rubani wa ndege hiyo ni zingine nje ya uwanja wa Cardiff City.

Gazeti la spoti la Ufaransa L’Equipe, limeangazia taarifa kuhusiana na Sala katika ukurasa wake wa kwanza: kwa kutumia maneno “Kutoweka kwa shujaa”.

iliandika: “Mjini Nantes, mashabiki walitumiana ujumbe wa kupeana nguvu.”

Ndege hiyo ya injini moja iliondoka Nantes, kaskazini mashariki mwa Ufaransa, saa moja na robo usiku wa Jumatatu na ilikua ikipaa umbali wa fiti 5,000 ilipowasiliana na waelekezi wa ndege wa Jersey ikiomba kutua.

Ilipoteza mawasiliano ilipokua umbali wa fiti 2,300 na baadae kutoweka kwenye rada ikiwa katribu na mji wa kaskazini magharibi wa Alderney.

Uchungiz umeanzishwa kubaini ni kilichokumba ndege hiyo.


Ramani inayoonesha mji wa Alderney na lighthouse

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents