Burudani

Matumaini yarejea tena kuhusiana na afya ya Bobbi Kristina – Ripoti

Hatimaye kumekuwepo na taarifa za kutia moyo kuhusiana na afya ya Bobbi Kristina Houston Brown Jumanne hii.

Bobbi Kristina Brown attends the opening night of "The Houstons: On Our Own" in New York

Shangazi yake, Leolah Brown, ambaye ni dada wa baba yake na Bobbi, Bobby Brown, amethibitisha kupitia mahojiano exclusive na Fox 5 Atlanta, kuwa madaktari wameiambia familia kuwa afya ya msichana huyo inaendelea kuimarika japo ameendelea kuwepo kwenye mashine inayomsaidia kuishi.

“Tunafahamu kuwa anafungua macho yake,” Leolah alisema. “Hiyo ni kweli. Anafungua macho yake na kuna mambo mengi zaidi anayofanya lakini Krissi anaendelea vyema sasa.”

“Kuna dalili nyingi zinazotuonesha kuwa atapona licha ya kile watu wanachokisema kwenye Internet,” aliongeza Leolah. “Krissi hajambo.”

Jana kuliandikwa taarifa kuwa familia yake imekubali kuwa imtolee Bobbi mashine ya kumsadia kuishi Jumatano hii siku ambayo wanaadhimisha kifo cha Whitney Houston.

Kupitia mwanasheria wake, Christopher Brown, Bobby Brown amevishutumu vyombo vya habari kwa kueneza habari za uzushi kuhusiana na afya ya mwanae:

We support the candlelight vigil for Bobbi Kristina. The Brown family is amazed by the love and support from all that attended. However the false reports that continue to appear in print and on the internet are egregious, false and will be dealt with at an appropriate time. In particular, the false reporting of TMZ, The National Enquirer, The Atlanta Journal Constitution and the Daily Mail (UK) citing, police sources, family sources and Bobby Brown himself, will receive my attention. The desire to be “first” has clouded the judgment of many reporters as they forgo accuracy. This is a criminal investigation and the integrity of that process requires silence.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents