Tupo Nawe

Matumizi ya Bangi bado changamoto Tanzania, Mara na Tanga vinara kwa uzalishaji

Matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi, yametajwa bado ni tatizo nchini, huku mkoa wa Mara ukiwa ni kinara katika kulima cha zao hilo ikifuatiwa na Tanga.

Image result for jenista mhagama"
Jenista Mhagama

Hayo yamesemwa bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya dawa za kulevya kwa mwaka 2018.

Pamoja na jitihada zilizofanywa na serikali katika kupambana na dawa za kulevya nchini, bangi imeendelea kuwa tatizo kubwa nchini, mikoa ambayo inaonekana kuathirika zaidi na kilimo cha bangi ni pamoja na Mara, Tanga, Morogoro, Arusha, Kagera na Ruvuma,” alisema Mhagama na kuongeza.

Kwa kipindi cha mwaka 2018 juhudi za vyombo vya dola kwa kushirikiana na wananchi zilifanikisha ukamataji wa tani 24.3 za bangi zikiwahusisha watuhumiwa 10,061.

Muhagama amesema katika kipindi cha mwaka 2018, kesi 7,592 zikiwa na watuhumiwa 10,979, zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali, kesi 7,174 zilizowahusisha watuhumiwa 11,045 ziliendelea kusikilizwa.

Serikali imeendelea kutoa huduma za tiba kwa watumiaji wa dawa za kulevya, jumla ya vituo sita vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Dodoma viliendelea kutoa huduma, hadi mwaka 2018 zaidi ya watumiaji 8,000 waliendelea kupatiwa huduma za Methadone katika vituo husika,” alisema Mhagama.

Naye, Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Dkt. Peter Mfisi, alisema serikali hainunui dawa za Methadone bali zinanunuliwa na wafadhili kutoka Canada na thamani yake ni Dola za Marekani 1,500 kwa kilo moja.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW